
MBUNGE wa Embakasi Mashariki, Babu Owino ametoa ushauri kwa wanafunzi huku wanaporejea shuleni baada ya likizo fupi ya katikati mwa muhula wa kwanza.
Akizungumza bungeni wakati wanafunzi wa shule moja kutoka
Embakasi walipozuru majengo ya bunge, Owino ambaye alipewa nafasi ya kutoa
ushauri kwa wanafunzi hao na naibu spika Gladys Shollei aliwataka kutoendekeza
mapenzi masomoni.
Owino alitumia lugha fiche kuwataka kuzingatia zaidi kalamu
na vitabu vyao badala ya kukumbatia na kubusu wenzao wa jinsia tofauti shuleni.
“Kwa niaba ya mheshimiwa
Mawathe, ningependa kuchukua nafasi hii kuwakaribisha wanafunzi kutoka Eneobunge
la Embakasi Kusini na ninataka kuwapa neno la ushauri kama watoto wetu,” Owino alisema.
“Elimu ndio njia pekee
kuelekea mafanikio. Mizizi ya masomo ni michungu lakini matunda yake ni matamu.
Wavulana kwa wasichana kumbuka ukiwa shuleni sasa hivi zingatia kwenye vitabu
na kalamu.”
“Kama utambusu mwanamume,
basi busu kitabu. Na kama utamkumbatia mwanamke basi kumbatia kalamu. Hicho ndicho
kitu pekee ambacho kitakuokoa kutoka katika lindi la umaskini,” Owino aliongeza.
Video hiyo hiyo ambayo imevutia maoni mengi ya vichekesho
ndio hii hapa chini;