logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Babu Owino amwandikia barua Rais Samia Suluhu

Matokeo haya yasiyotarajiwa yalimfanya mbunge huyo wa Kenya kulalamikia ukiukwaji wa haki yake

image
na Japheth Nyongesa

Yanayojiri04 February 2025 - 11:13

Muhtasari


  • Babu kwenye barua ambayo ameituma kupitia ubalozi wa Kenya nchini Tanzania akielekeza moja kwa moja kwa Rais wa nchi hio  Samia Suluhu amemurai Rais huyo kumujibu kupitia maandishi.
  • Owino ametaka yaorodeshwe maswala ambaye yamefanya yeye kufungiwa mipaka kuingia nchini mwake.

Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu owino amemwandikia Barua rais wa Tanzania Samia Suluhu akitaka kujua chanzo cha yeye kufungiwa kuingia nchini humo.

Babu kwenye barua ambayo ameituma kupitia ubalozi wa Kenya nchini Tanzania akielekeza moja kwa moja kwa Rais wa nchi hio Samia Suluhu amemurai Rais huyo kumujibu kupitia maandishi maswala ambaye yamefanya yeye kufungiwa mipaka kuingia nchini mwake.

"Naandika ili nikuelezee kwamba nilipotembelea Tanzania hivi karibuni Desemba 2024 baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Dar es Salaam, maafisa wenu wa uhamiaji walikataa pasipoti yangu na kuniarifu kwamba jina langu lipo kwenye orodha ya watu wasio na grata nchini Tanzania," Owino aliandika.

Matokeo haya yasiyotarajiwa yalimfanya mbunge huyo wa Kenya kulalamikia ukiukwaji wa haki yake sio tu kama raia wa Afrika Mashariki bali pia kama mwakilishi wa Bunge la Kenya ambalo linampa haki ya kuingia Tanzania.

"Kwa kukiuka kabisa haki zangu za uhuru wa kutembea, walinikamata kwa muda katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere."

"Mimi ni raia wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, hasa Kenya, kwa jambo hilo. Mimi ni mbunge wa Bunge la Kenya, ambalo linawakilishwa kihalali katika EALA, ambalo kiti chake kiko Tanzania," barua yake iliendelea.

"Azima ya Ulimwengu ya Haki za Binadamu na Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa (ICCPR) unahakikisha haki za watu za kuingia na kutoka katika mataifa baada ya kufuata mchakato unaofaa, jambo ambalo nilifanya."

"Mwisho, Kenya, kama taifa huru, inatoa pasipoti za kusafiri kwa raia wake, ambazo zinatambuliwa na mataifa mengine chini ya sheria za kimataifa. Haki hizo zote na uhuru wa msingi unanihusu mimi kama raia wa sayari hii," alihitimisha.

Kwenye barua Babu alieleza kuwa Mkataba wa Afrika Mashariki na Kanuni za Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki (Free Movement of Persons) zinatoa uhuru wa kusafiri kwa raia wa nchi washirika.

Jumamosi, Februari 1, mbunge huyo aliandika ujumbe kwamba alikuwa amezuiliwa kwa saa tatu katika uwanja wa ndege kwa madai kuwa alikuwa kwenye orodha ya watu wanaotafutwa zaidi nchini Uganda na Tanzania.

"Nilienda Tanzania, na nilipofika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam na kutoa pasi poti yangu ya kusafiri ili nipiahwe na uhamiaji, nilishtuka kuona jina langu limeorodheshwa kama mmoja wa watu walio kwenye orodha ya watu wanaotafutwa na 'Interpol," Babu Owino alikuwa amefichua kabla ya kuandika barua.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved