
YOUTUBER na Rapa Diana Marua alinusurika kung’atwa na mbwa wake mguuni baada ya jaribio la kutaka kucheza na mbwa huyo kuenda fyongo.
Katika video ambayo alichapisha kwenye
YouTube yake Ijumaa ya Machi 15, Marua ambaye alikuwa amevalia mavazi meusi
alionekana akimkaribia mbwa huyo wanayemuita ‘Coco’.
Alikuwa akieleza mpango jinsi wanawe
watakuwa wanamtoa mbwa wao kwenye nyumba yake mara kwa mara kwa ajili ya
kumpigisha misele nje.
Hata hivyo, watoto hao walionekana kupinga
wazo hilo tangu mwanzo, huku binti yake Heaven akilipinga kwa kauli kwamba
mbwa wa familia ni mkali na anaweza dhuru watu.
Mama yao aliyeonekana kutoamini kauli za
mwanaye kwamba mbwa wa familia ni mkali alitaka kuwaonyesha jinsi mbwa huyo ni
rafiki kwa kila mtu – lakini jaribio lake nusra limsababishie kung’atwa.
kwa ujasiri alimuamuru mfanyakazi wao mmoja
amwachie huru, lakini kabla hata mlango wa banda la mbwa haujafunguka, tayari
watoto wake wote walikuwa wameshaingia ndani ya nyumba hiyo, na kumwacha Diana
pekee ambaye ndiye aliyekuwa akimwonea huruma mbwa huyo, akiwa amesimama peke
yake pale nje.
Wakati Coco alipoachiliwa, jambo
lililomshtua sana Diana, badala ya kutoka nje kwa utulivu ili kufurahia uhuru
wake, mbwa huyo alimfungia macho, akiwa na kasi kubwa, akibweka kwa hasira huku
akimjia Diana kwa kasi.
Diana alijaribu kukwepa kasi ya mbwa wake
ambaye alionekana kuwa na azma ya kufikia kisigino chake au paja lakini kwa Bahati
nzuri, mfanyikazi wake ambaye alikuwa amemfungulia mbwa huyo alifika na
kumzuia.
Marua alibaki katika hali ya mstuko na
kutetemeka huku akiishiwa na maneno kinywani.
Baada ya kujikusanya Pamoja, Diana
alikubaliana na wanawe kwamba mbwa huyo ni hatari kwa usalama wao pale nyumbani
na kutoa maoni kwamba huenda wakawazia kumuuza ili kuleta mbwa mwingine
mkarimu.