
Mangale ameeleza kwamba baada ya kuacha masomo jambo lililomfanya kufungwa jela wakati angali na umri mdogo na kuanza kujihusisha na kukahaba baada ya kutoka korokoroni.
"Ningerudi msichana mdogo sai , ningesoma. Hii dunia kila kitu ni kusoma. Tulikuwa kikundi kimoja. Fikiria hii timu hamjasoma, mlikataa shule, mmepelekwa college mmekataa. Mnataka vitu za harakaharaka, kama ni nguo ya wenyewe kwa kamba tunatoa, kama ni kiatu ya wenyewe unaanua. Inafika mahali unanunua ghamu, unatoka hurumaa mguu mpaka mlango kumi. Kiini unataka usionekane wewe ni fala,"alieleza mchungaji Wangale.
"Ikapata tumeingia maisha ya kuvuta ghamu, tukashikwa tukiwa na umri mchanga. Tukashitakiwa kwa kosa la ukahaba kwa sababu tulipatikana kwa bar. Baada ya kukaa kwa jela nikamaliza nikatoka na nikakuwa raia nikanyamaza nyumbani sitoki inje nikakuwa mtoto mzuri. Sasa wale marafiki zangu wa zamani wanapita hapo wanasema Kioga kilishikwa sasa hakitokangi kwa nyumba. Baadaye nikaamua si nishakuwa X - Langata si nitoke ndo nioneshe mimi sio muoga,"mchungaji huyo aliendelea kueleza.
"Nikatoka nikaenda tafrija na huko kila mtu na mtu wake, nikaenda kwa mjamaa nikapata nimeolewa, kidogo nikapata mimba, nikajaribu kutoa hiyo mimba ikakataa. Tukaa na huyo jama wangu kidogo nikanyang'anywa na suger mami," aliweka wazi masaibu yake aliyokumbana nayo.
Mchungaji huyo pia aliongeza kwamba rafiki yake wa karibu ambaye alidhani angemsaidia naye alimuzidishia shida na kumuingiza kwenye ukahaba na kudai anamsaidia.
"Baada ya kulezea rafiki yangu akaniambia nitkupeleka kazi. Mimi nikajua kazi ni ya ofisi. Ikakua wakati wa kutoka akaniambia wewe pea mtoto pritoni alale. nikajikuta Koinange streat nikapata watu wanavaa mini skirt nikaambiwa hii ndio job. Siku za kwanza tatu sikutafuta pesa. huyo rafiki akaniambia kama hutaki kutafuta pesa tembeza. Vuta bhangi, kunywa pombe utoe uwoga ili upate kuita hao majamaa," alifichua.