
MZEE wa kanisa anadaiwa kuzirai na baadae kufa kanisani wakati wa ibada ya kusherehekea heri njema ya miaka 60 ya kuzaliwa kwa mke wake.
Katika video ambayo imezua minong’ono mingi kwenye mitandao wa
X, mzee huyo ambaye alionekana mwingi wa furaha aliongoza marafiki wa karibu
kwenye mimbari kuimba nyimbo za furaha kwa mkewe kufikisha umri wa miaka 60.
Mara kwa mara, mkewe ambaye alikuwa anacheza densi kando yake
alionekana akimnong’onezea huku wote wakitabasamu kwa zamu.
Hata hivyo, dakika chache baadae, mzee yule aliweka kipaza
sauti juu ya meza na kuonekana kuanguka kwenda nyuma.
Waliokuwa wamemzingira walifanya hima kumshikilia kabla ya
kutua sakafuni na kuanza kumpa huduma ya kwanza, na hata hivyo alisemekana
kufariki dakika chache baadae.
Baadhi ya watu katika maoni yao walihisi tukio lililomkumba
mzee wa watu kuna uwezekano mkubwa chanzo chake ni ugonjwa wa shinikizo la
damu.
Haya hapa baadhi ya maoni;
@Ekene_Chigozie: “Pima shinikizo la Damu kila wakati.”
@iamizuogu: "Mama mwenye nyumba mwingine aliongeza.
Baada ya wanaume kujishughulisha wenyewe hawataishi kamwe kula matunda ya kazi
zao. Inasikitisha mama mwenye nyumba kila mahali."
@EsioUweh: "Maisha hayatabiriki sana. Hata wakati wa
msisimko lolote linaweza kutokea."
Tazama video hiyo hapa kisha utoe maoni yako;