
MHUDUMU wa teksi aliwashangaza watangazaji wa kipindi redioni alipopiga simu akitaka msaada wa kusaidiwa kumpata mteja wake aliyesahau kitita cha pesa katika gari lake.
Hii ilifichuliwa katika video inayovuma kwenye TikTok, ambapo
kitendo cha nadra cha dereva kilipongezwa.
Kwa mujibu wa dereva huyo wa teksi, alimpa mteja huduma ya
kumsafirsha hadi alikotaka na baada ya kushuka na kutokomea, aligundua mfuko wa
mteja huo katika kiti cha nyuma.
Dereva huyo aliufungua mkoba ule na kwa kustaajabu alipata
kitita cha dola laki moja – sawa na shilingi 12,995,000.
Akiwa amechanganyikiwa, dereva huyo alikwenda redioni kutaka
kusaidiwa ujumbe wake kutangazwa ili kumfikia mteja wake, ambaye alihisi
pengine pia alikuwa anataabika kuipata teksi ile aliyoabiri.
Hadithi hiyo ilipozidi kuvuma mtandaoni, watu wengi
walifurika sehemu ya maoni ili kumpongeza dereva kwa uaminifu wake wa ajabu.
Wengine hata hivyo walimdhihaki kwa kile walihisi ni kuitupa
baharini bahati yake na kudai kwamba huenda akaishi milele kuwa maskini.
Tazama baadhi ya maoni hapa chini:
@ezemalonginusuche: “mtu wa teksi atabaki kuwa maskini kwa
vile hawezi kutumia nafasi ambayo Mungu amempa, mtu anayesahau dola 100,000
lazima apate dola 500,000 nyingine.”
@Daniel Ogbu Jr.: "Ni vipi mtu anavyoweza kushikilia
$100k wakati yeye anatumia teksi... ikiwa yeye mwenyewe ni mwizi."
@Flexy: "Karibu kila mtu anamtukana huyu mtu. Hebu
niambie mwanaume huyo atakuwa na amani ya akili kwa kufanya jambo sahihi.
Nimefanya vivyo hivyo nilipokuwa kijana, begi lenye pesa."
@Enshi_Sheriff: "Ni kama vile utajiri huu wa kizazi
unaanza, na mwizi mmoja mkubwa."
@Da Modest: “MUNGU anisamehe😏😭 lakini dereva wa teksi
hawezi kuwa tajiri tena maishani ☹️☹️ikiwa Mungu anaweza kutumia samaki kusaidia mtu, bado uko
huru kumwongoza baraka zake 😩😩.”