
MORGAN Bahati, mtoto wa kiasili wa msanii Bahati Kioko na Diana Marua amemshangaza mamake kwa kukiri kwamba amekuwa akitumia midomo yake kubusu.
Akizungumza na Diana Marua katika kipindi cha maswali na
majibu kwenye Chaneli yake ya YouTube, Morgan alikiri kwamba amekuwa akibusu
msichana mmoja tu lakini kwa mara kadhaa.
Tineja huyo alijitetea kwa hatua hiyo akitania kwamba midomo
yake inapendeza mno kiasi kwamba hawezi kukosa kuitumia katika kutoa busu la
kimahaba kwa mpenzi wake.
Alipoulizwa ni mara ngapi amebusu msichana, Morgan alisema
kwamba anaweza hesabu ni mara ngapi lakini baadae akadai kwamba imefanyika mara
kadhaa japo kwa msichana mmoja tu.
“Umewahi busu msichana?” Diana Marua alimuuliza
Morgan.
“Ndio! Angalia katika hii
midomo mikubwa, ilitengenezwa ili kutotumika ipasavyo? Nimebusu ndio lakini sio
katika hii shule, ni katika shule ya Juja.”
“Ukweli ni kwamba
nimebusu na si mara moja, japo naweza hesabu ni mara ngapi…jambo zuri ni kwamba
nimefanya mabusu kadhaa kwa msichana mmoja,” alisema.
Kijana huyo alieleza kwamba kabla ya kuondoka katika shule ya
Juja mwishoni mwa 2023, yeye na mpenzi wake katika shule hiyo ambaye alibusu
mara kadhaa walifanya maagano kwamba hakuna mmoja kati yao atakuwa na mpenzi
mwingine licha ya wao kutokuwa pamoja tena.
“Wakati nilikuwa naondoka
kule, tulikuwa tunafunga shule muhula wa 3 mwaka 2023. Tulifanya maagano kwamba
hakuna atakayekuwa na mpenzi mwingine na tangu wakati huo mimi nimeheshimu
makubaliano hayo kwani sijakuwa na mpenzi mwingine.”
“Japo nina namba yake ya
simu, huwa hatuzungumzi na hata sijui kama alisonga mbele na maisha yake. Lakini
hatumai bado. Nikigundua kwamba alipiga hatu kimaisha, nitahuzunika,” Morgan alijieleza.