
KEVIN Kioko maarufu kama Bahati ametangaza mpango wa kumnunulia mkewe, Diana Marua zawadi nyingine ya gari la kifahari.
Kupitia Instagram, Bahati alitoa maoni
chini ya chapisho la Diana Marua ambaye alionyesha kuridhika na maisha
anayopewa na mumewe kwa zawadi kochokocho.
Diana alionyesha gari aina ya Brabus
ambalo Bahati alimpa wiki kadhaa zilizopita kama moja ya zawadi ya kusherehekea
takribani muongo mmoja wa uhusiano wao.
“Diana Brabus, nitakuwa nadanganya kama
nitasema maisha si mazuri,” Diana aliandika.
Akijibu, Bahati alisema kwamba gari
hilo kwa vile limekuwa moja ya mada zilizozungumziwa sana katika mitandao ya
kijamii, anapanga kumnunulia gari lingine la kifahari aina ya Lamborghini
“Hili gari limegonga vichwa vya habari
sana, zawadi itakayofuata ni ya gari aina ya Lamborghini,” Bahati aliandika.
Mwishoni mwa Februari, Bahati alifanya
kufuru ya karne kwa kumnunulia mkewe zawadi ya gari la pink la Brabus ambalo
lilitajwa kuwa lenye thamani ya zaidi ya milioni 45 pesa za Kenya.
Gari hilo lilikuwa kelele cha jumla ya
zawadi nane ambazo msanii huyo alimpa mkewe kama ishara ya kumshukuru na kumthamini
kwa miaka 8 ya uhusiano wao ambapo wamebarikiwa na watoto 3.
Wawili hao walivalia mavazi ya waridi
yaliyofanana, bila kujua kuwa mwanamuziki huyo alikuwa amenunua gari aina ya
G-Wagon Brabus.
Bahati alifichua kuwa gari hilo
lilikuwa na thamani ya KSh 45 milioni lilikuwa limeboreshwa kulingana na rangi
ya waridi ya Diana.
Alianguka chini na kulia baada ya
mumewe kufunua gari.