
Seneta wa kuteuliwa Karen Nyamu amedokeza kuwa tayari ameachana na mwanamuziki tajika wa Mugithi, Samuel Muchoki, almaarufu Samidoh.
Kwa muda sasa, kumekuwa na tetesi kuhusu uhusiano wao kuvunjika kimyakimya, lakini hakuna aliyewahi kuthibitisha hilo hadharani. Hata hivyo, Nyamu sasa amedokeza kuwa uhusiano wao haukufaulu licha ya wao kupata watoto wawili pamoja.
Akizungumza katika kipindi cha moja kwa moja mtandaoni na Mbunge wa Gatundu Kaskazini, Elijah Kururia, Bi Nyamu alidai kuwa alimuacha Samidoh kwa sababu alishindwa kushughulikia mambo vizuri.
“Huyo alishindwa. Nillimfuta kazi. Alishindwa kabisa. Yeye ni wa kuonewa huruma tu. Watu hawawezi kuniuliza kwa nini kwa sababu wanajua, wameona kila kitu na bado wanaona,” Nyamu alimwambia Kururia.
Wawili hao walikuwa wakijadili kuhusu mahari, ambapo Kururia alimuuliza Nyamu ikiwa Samidoh ndiye aliyekuwa akipanga kumlipia mahari.
Katika majibu yake, Nyamu alisema kuwa Kururia alimshawishi akubali kulipiwa mahari na akadokeza kuwa mwanamume mwingine, si Samidoh, ndiye atakayelipa.
“Nimekuwa nikisema sitalipiwa mahari. Lakini yeye (Kururia)
amenishawishi kuwa si jambo baya. Kwa sababu yake, sasa nimejielewa. Na mpenzi
wangu ataona mabadiliko,” alisema.
Miezi michache iliyopita, Nyamu alionekana kthibitisha kuwa yuko kwenye uhusiano wa kimapenzi mzito sana.
Mwanasiasa huyo alikuwa hospitalini katika siku chache
zilizopita alithibitisha kuhusu hali yake ya uhusiano katika kipindi cha moja
kwa moja cha hivi majuzi kwenye mtandao wa Facebook.
Kutoka kwa kitanda chake hospitalini, alifichua kwamba kwa
miezi saba hivi iliyokuwa imepita alikuwa akichumbiana na mwanamume ambaye alimtaja
kuwa mwenye upendo sana.
“Mimi si single. Sijawa single tangu Juni mwaka huu,” Karen
Nyamu alisema.
Seneta huyo alifichua hayo alipokuwa akimjibu shabiki aliyedai
kuwa alikuwa na mchubuko machoni, ishara ya ukatili wa kijinsia.
Nyamu hata hivyo alikanusha madai ya kupigwa na mpenzi wake
akibainisha kuwa mwanamume anayechumbiana naye hawezi kumshambulia hata kidogo.
“Nina mwanaume anayenipenda sana. Huyo labda anipige busu,
hawezi kunipiga. Niko na chali mtrue sana, nashukuru Mungu. Mimi si single,”
alisema.
Jibu la Karen Nyamu pia lilionekana kuthibitisha kwamba sasa
anachumbiana na mwanamume mwingine baada ya kudaiwa kutengana na mzazi mwenzake
Samidoh.