logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kituo cha polisi chageuka eneo la vita wanawake 6 wakipigania mwanamume mmoja

Wanawake wote walikasirika na kukata tamaa kugundua kwamba mwanamume ambaye alikuwa ameahidi ndoa kwa kila mmoja wao pia alikuwa akiwagawa soseji yake ya kibaolojia kwa wengine.

image
na MOSES SAGWEjournalist

Dakia-udaku08 April 2025 - 15:18

Muhtasari


  • Mwanamume aliye katikati ya zogo hilo alitambulishwa kwa jina la Andrew, mwenye umri wa mia,a 31.
  • Sasa anakabiliwa na mashtaka ya kughushi, kutoa stakabadhi za uongo na wizi kwa kutumia udanganyifu na ujanja wenye hasara.

Pingu

KITUO kimoja cha polisi kiligeuka eneo la mzozo mkali wa vita wakati wanawake 6 walijitokeza kituoni humo kila mmoja wao akidai mwanamume aliyekamatwa na polisi ni mume wake.

Katika video hiyo ambayo imezua minong’ono kwenye mitandao ya kijamii, inaarifiwa kwamba mwanamume huyo alikamatwa na wake wake wa karibu wakamtembelea kwa lengo la ‘kununua’ uhuru wake kurudi uraiani.

Hata hivyo, tukio lisilotarajiwa lilitokea wakati wanawake 6 walijitokeza kila mmoja akidai kwamba huyo ni mume wake – cha ajabu ni kwamba 2 walikuwa wajawazito.

Wanawake sita ambao walithibitisha kwa maafisa kwamba wote walikuwa wamechumbiwa na mwanamume mmoja waliunda uwanja wa michezo wa karate huku wakibanana na kuvuta nywele za kila mmoja kwa sauti ya matusi.

Maafisa, ambao walikuwa mashahidi wa kwanza wa tamthilia hiyo waliachana na majukumu yao kwa muda kuwatenganisha maharusi wanaopigana.

Wanawake wote walikasirika na kukata tamaa kugundua kwamba mwanamume ambaye alikuwa ameahidi ndoa kwa kila mmoja wao pia alikuwa akiwagawa soseji yake ya kibaolojia kwa wengine.

Mwanamume aliye katikati ya zogo hilo alitambulishwa kwa jina la Andrew, mwenye umri wa mia,a 31.

Polisi waligundua kwamba Andrew alikuwa akiendesha mnara wa ndoa ghushi akiahidi kila mwanamke aliyeingia kwenye kumi na nane zake kwamba angemuoa katika kile alichokiita ‘muda mwafaka’.

Inasemekana wanawake hao watano walikuwa wamepoteza maelfu ya michango ya benki ya kijiji ambayo walimkopesha mume wao mtarajiwa ambaye alidanganya kwamba alitaka kutumia pesa hizo kuandaa harusi.

Inaaminika pia kuwa Andrew aliwalenga kimkakati wanawake wazee waliokata tamaa ya mapenzi na usuhuba kwa kukandamiza matumaini yao kwa umri uliotawaliwa na kuwaambia kuwa alizaliwa mwaka wa 1991 wakati ukweli ni kwamba mwanamume huyo alikuwa mtoto mchanga aliyetengenezwa mwaka wa 1994, na kuwathibitishia wanawake hao kwamba mjini ni pa biashara na si mapenzi.

Sasa anakabiliwa na mashtaka ya kughushi, kutoa stakabadhi za uongo na wizi kwa kutumia udanganyifu na ujanja wenye hasara.

 

 

 

 

Polisi wa Kabwata wametoa wito kwa mtu mwingine yeyote aliyetapeliwa na Mario Promax kujitokeza.

 

Ripoti pia zinaonyesha kuwa Kosamu ana kesi zinazoendelea katika vituo vingine vya polisi kote Lusaka.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved