logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Raha yageuka karaha: Mfanyibiashara azirai na kufa katika mchezo wa kufungwa wakati wa kufanya mapenzi

Mwanaume huyo alifurahia mateso hayo mwanzoni, lakini dakika 15 baada ya kunyongwa, alianza kupoteza fahamu.

image
na Samuel Mainajournalist

Kimataifa07 March 2025 - 10:34

Muhtasari


  • Mteja alilipa takriban Sh140k  kwa ajili ya kipindi hicho, ambacho kilihusisha mbinu mbalimbali za kufungwa na kunyongwa kwa minyororo ya chuma.
  • Jacqueline, ambaye ni mtaalamu wa michezo ya kufungwa wakati wa mapenzi, alijaribu kumrejesha mteja wake katika hali ya kawaida bila mafanikio.

Tendo la ndoa

Kipindi cha michezo ya kufungwa wakati wa mapenzi kimegeuka janga baada ya mfanyabiashara mmoja kufariki kutokana na kunyongwa kwa minyororo katika kikao cha starehe kilichodumu kwa saa sita.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Ujerumani, mfanyabiashara huyo (ambaye jina lake halijawekwa wazi) hivi majuzi alihudhuria kipindi cha kimapenzi kilichoendeshwa na mwanamke anayetawala katika michezo ya kimapenzi, Jacqueline S., mwenye umri wa miaka 50.

Mteja huyo alilipa takriban pauni 750 (takriban KSh 140,000) kwa ajili ya kipindi hicho, ambacho kilihusisha mbinu mbalimbali za kufungwa na kunyongwa kwa minyororo ya chuma.

Katika kipindi hicho, mfanyabiashara huyo alivishwa korseti kali, akafungwa mikono yake, na hatimaye akatundikwa kwa kutumia minyororo na ndoano iliyokuwa imeshikilia sehemu za mwili wake.

Kwa mujibu wa taarifa, mwanaume huyo alifurahia mateso hayo mwanzoni, lakini dakika 15 baada ya kunyongwa, alianza kupoteza fahamu.

Jacqueline, ambaye ni mtaalamu wa michezo ya kufungwa wakati wa mapenzi, alijaribu kumrejesha mteja wake katika hali yake ya kawaida lakini bila mafanikio.

Alipogundua kuwa hali ilikuwa mbaya, aliwaita wahudumu wa dharura waliomkimbiza hospitalini. Hata hivyo, siku tatu baadaye, mfanyabiashara huyo alifariki kutokana na matatizo ya kupumua na shinikizo la damu lililotokana na kunyongwa.

Baada ya kifo hicho, polisi walimkamata Jacqueline kwa kosa la kusababisha madhara makubwa yaliyopelekea kifo.

Sheria za Ujerumani zinamtuhumu kwa kulegea katika mchezo huo wa kimapenzi, na ikiwa atapatikana na hatia, anaweza kufungwa kwa angalau miaka mitatu gerezani.

Tukio hili limezua mjadala mkali kuhusu usalama wa michezo ya kufungwa wakati wa mapenzi na mipaka ya ridhaa kati ya wahusika. Wataalamu wa masuala ya ngono na mahusiano wanatoa tahadhari juu ya hatari zinazoweza kutokea ikiwa hatua za usalama hazitachukuliwa.

Kwa sasa, uchunguzi wa tukio hili bado unaendelea, huku Jacqueline akisubiri hatima yake mahakamani. Wakati huo huo, jamii ya Hamburg imesalia na mshangao wa jinsi starehe ilivyogeuka kuwa janga la mauti.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved