logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kutotahiriwa hakupunguzi utamu wa mapenzi - Suzanna Owiyo atoa kauli tatanishi kuhusu tohara

Owiyo amesisitiza kuwa wanawake ndio wenye nafasi bora zaidi kuelezea iwapo tohara ni ya maana au la.

image
na Samuel Mainajournalist

Dakia-udaku05 March 2025 - 11:06

Muhtasari


  • Owiyo amesisitiza kuwa wakati wa mapenzi hakuna tofauti kati ya mwanaume aliyetahiriwa na asiyetahiriwa.
  • "Nitawaambia tu kwa urahisi, shimo ni shimo. Shimo halitambui kitu kilichokatwa na kile kisichokatwa," alisema.

caption

Msanii mashuhuri wa muziki wa Benga, Suzanna Owiyo, amejiunga na mjadala unaoendelea kuhusu umuhimu wa tohara kwa wanaume.

Mjadala kuhusu tohara na umuhimu wake umekuwepo kwa muda mrefu, lakini umechukua sura mpya nchini Kenya hivi majuzi baada ya Mbunge wa Homa Bay Town, Peter Kaluma, kutoa wito wa kufutwa kwa desturi hiyo.

Akiizungumzia hoja hiyo kupitia video aliyochapisha kwenye mitandao ya kijamii, Suzanna Owiyo alisisitiza kuwa wanawake ndio wenye nafasi bora zaidi kuelezea iwapo tohara ni ya maana au la.

"Kuna hadithi iliyochoka kuhusu tohara. Kitu ambacho watu wanashindwa kuelewa ni kwamba wanawake wako kwenye nafasi bora zaidi ya kueleza haya yote," Owiyo alisema kwenye video hiyo.

Alibainisha kuwa tohara haina umuhimu wowote katika tendo la ndoa, akisisitiza kuwa hakuna tofauti kati ya mwanaume aliyetahiriwa na yule ambaye hajatahiriwa.

"Nitawaambia tu kwa urahisi, shimo ni shimo. Shimo halitambui kitu kilichokatwa na kile kisichokatwa. Ulizeni wanawake, maana ninajua wengi wao wameonja vyote viwili. Unachofanya na taarifa hii si jukumu langu. Kazi kwenu," alisema.

Mjadala kuhusu tohara kwa wanaume umekuwa na mitazamo tofauti, hasa kutoka kwa madaktari, wanaharakati wa haki za binadamu, viongozi wa dini, na jamii kwa ujumla.

Tohara imekuwa ikihusishwa na sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na usafi wa mwili, afya ya uzazi, na mila za kijamii na kidini.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limewahi kueleza kuwa tohara inaweza kusaidia kupunguza hatari ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa, ikiwa ni pamoja na Virusi vya Ukimwi.

Hata hivyo, kuna wanaharakati wanaoipinga, wakisema kuwa ni desturi isiyo ya lazima na kwamba wanaume wanapaswa kupewa uhuru wa kuamua kuhusu miili yao.

Kauli ya Suzanna Owiyo imezua hisia mseto mtandaoni, huku baadhi ya watu wakikubaliana naye na wengine wakipinga mtazamo wake vikali.

Wakati mjadala huu ukiendelea, swali linabaki: Je, tohara ni ya lazima kwa wanaume, au ni suala la uchaguzi binafsi?

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved