logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Sehemu ya Barabara Kuu ya Thika Kufungwa Kwa Siku 4

Hatua hii imechukuliwa ili kuruhusu ujenzi wa daraja jipya la watembea kwa miguu.

image
na Samuel Mainajournalist

Yanayojiri15 February 2025 - 10:58

Muhtasari


  • KeNHA imetangaza kufungwa kwa muda kwa sehemu ya barabara ya Thika Superhighway katika eneo la Juja Highpoint.
  • Wale wanaoelekea Thika watatumia mzunguko ulio nyuma ya Hoteli ya Centurion kabla ya kuungana tena na barabara kuu.

Thika Road.

Mamlaka ya Barabara Kuu ya Kenya (KeNHA) imetangaza kufungwa kwa muda kwa sehemu ya barabara ya Thika Superhighway katika eneo la Juja Highpoint, maarufu kama Centurion.

 Kulingana na taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa KeNHA, Eng. Kung’u Ndungu, barabara hiyo itafungwa kwa siku nne kuanzia Jumamosi, Februari 15, 2025, hadi Jumanne, Februari 18, 2025, kati ya saa tano usiku na saa kumi na mbili asubuhi.

 Hatua hii imechukuliwa ili kuruhusu ujenzi wa daraja jipya la watembea kwa miguu.

 Madereva wanaoelekea Nairobi wametakiwa kutumia barabara ya mzunguko iliyo nyuma ya kituo cha mafuta cha Lex Petrol kabla ya kuungana tena na Thika Superhighway.

 Vilevile, wale wanaoelekea Thika watatumia mzunguko ulio nyuma ya Hoteli ya Centurion kabla ya kuungana tena na barabara kuu.

 KeNHA imetoa wito kwa madereva kuwa waangalifu wanapopita karibu na eneo la ujenzi, kufuata mpango wa usimamizi wa trafiki uliopendekezwa.

 Watumizi wa barabara pia wametakiwa kushirikiana na maafisa wa trafiki na maaskari wa usalama barabarani walioko eneo husika ili kuhakikisha mchakato unafanyika kwa utaratibu.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved