
Mwanamziki wa Kenya Bien-Aime Baraza amezungumzia safari yake ya Zanzibar kwa maara ya kwanza baada ya kushinda tuzo ya mwanamziki bora wa Afrika Mashariki huko nchini Tanzania.
Bien pia alitumia nafasi hiyo kueleza safari yake ya kimuziki huku akiahidi kusonga mbele katika tasnia ya kimuziki.
Alianza na kuelezea kwamba alipendezwa sana na safari yake ya kuelekea Zanzibar katika mapambano yako ya Trace Awards yanayohusisha wasani wa kila aina kutoka Afrika na nje ya Afrika.
"Wakati wangu Zanzibar ulikuwa mzuri, nilipata kuona wanamziki wengi sana. ambao wamekuwa wakiimba kwa miaka. nilipatana pia na marafiki wazuri. nikapatana na wanamziki wageni... nilikutana na kizazi kipya, kizazi cha zamani," alisema Bien.
Wakati huo huo pia Bien alitoa shukrani zake kwa usimamizi wa tuzo za Trace kwa kazi nzuri ya kuunganisha mziki wa Kiafrika na kuendelea kuukuza.
"Nataka kuwashukuru Trace... Trace ilifanyanya hili likawezekana. Na kwa pamoja tukaona kwamba Afrika iko katika mikono mizuri. Tasnia ya muziki wa kiafrika uko katika mikomo mizuri.
Ahsante sana Trace kwa kutupa nafasi sisi wote, na kushurehekea mziki wetu kwa kizazi hiki," alieleza mshindi huyo wa tuzo ya mwanamziki bora wa Afrika Mashariki.
Msanii huyo aliahidi kuendelea kutia bidii kwenye tasnia ya mziki huku akisema kwamba ndio safari yake ya kung'aa kwenye mziki inaanza.
Hata hivyo amewataka wafuasi wake kumuunga mkono ili kusonga katika hatua nyingine, hasa watu wa taifa lake la Kenya.
"Safari ndo imeanza tu. Huu ndo ushindi wangu mkubwa, kama mwanamziki mgeni. mkiniunga mkono mamzee, tunaeza enda mbali. Kwa hivyo tuendelee kufanyua hii kazi pamoja maana nawahitaji. Mwanzo hatukujua kwamba tunafanya kitu kizuri. Lakini ni kizuri," alifichua msani huyo.
Bien alitoa shukrani zake kwa watu wanaomuunga mkono. vile vile aliwahimiza wasani wachangaa kuendelea kutia bidii kwenye kazi zao.
"Kwa kila mtu ambaye hayuko hapa lakini alisaidia kufika kwangu hapa santi. Yule ambaye alisaidia na kujitokeza katika mziki wangu, shukrani. wote waliosaidia katika kuandika mziki wangu. shukrani. Imani na upendo unatoka kwangu," alikamilisha Bien.