logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Chameleone azungumzia afya yake baada ya safari ndefu ya matibabu, afichua somo maalum ugonjwa umemfundisha

Chameleone alizungumza baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kiafya katika Hospitali ya Massachusetts General, Marekani, Alhamisi asubuhi.

image
na Samuel Mainajournalist

Mastaa wako06 March 2025 - 04:34

Muhtasari


  • Chameleone, ametoa shukrani kwa mashabiki, marafiki, na serikali ya Uganda kwa msaada waliompa wakati wa kipindi kigumu cha ugonjwa wake.
  • Chameleone alisisitiza umuhimu wa urafiki wa kweli na afya, akisema kuwa ugonjwa wake umempa funzo kubwa.

Jose Chameleone akiwa hospitalini

Msanii maarufu wa Uganda, Jose Chameleone, ametoa shukrani kwa mashabiki wake, marafiki, na serikali ya Uganda kwa msaada waliompa wakati wa kipindi kigumu cha ugonjwa wake.

Kupitia ujumbe wake baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kiafya katika Hospitali ya Massachusetts General, Marekani, Alhamisi asubuhi, Chameleone alieleza kuwa anashukuru kwa maombi na upendo mkubwa aliopokea.

"Imekuwa safari ndefu, lakini tunashinda mabaya kwa upendo. Ninaamini na sitawahi kukosa matumaini kwamba Mkombozi wangu atanivusha daima! Utukufu kwa Mungu siku zote," aliandika Chameleone kwenye ujumbe wake wa shukrani aliochapisha Facebook

Mwanamuziki huyo, ambaye jina lake halisi ni Joseph Mayanja, alisafiri kwenda Marekani kwa ajili ya matibabu maalum baada ya hali yake ya afya kuzorota.

Ingawa hakufichua undani wa maradhi yake, ripoti za awali zilidai kuwa alikuwa akipambana na matatizo ya figo na maambukizi yaliyoathiri mwili wake kwa kiasi kikubwa.

Katika ujumbe wake wa Alhamisi asubuhi, alionyesha furaha kwa maendeleo aliyoyapata, akiwashukuru wote waliomuombea na kumuonyesha upendo.

"Nawashukuru wote kwa maombi ya kimya kimya mliyofanya kwa ajili yangu, nami pia nilijitahidi! Shukrani kwa madaktari na kwa wote ambao, bila shaka yoyote, walijua kwamba kwa namna fulani nitakuwa sawa," alisema.

Chameleone aliendelea kusisitiza umuhimu wa urafiki wa kweli na afya, akisema kuwa ugonjwa wake umempa funzo kubwa.

Alimshukuru Juliet na Julie kwa msaada mkubwa waliompa wakati wa kipindi chake cha ugonjwa.

"Kupitia hili, nimejifunza kuwa afya na urafiki ni vitu vya msingi maishani! Asante Juliet, Julie, wewe ni Malkia na shujaa katika hili, na usiache kamwe kufanya wema hata kwa wengine," aliandika.

Chameleone pia hakusita kuonyesha shukrani zake kwa serikali ya Uganda kwa mchango wao katika safari yake ya afya.

"Serikali ya Uganda, asante sana," alisema kwa msisitizo mkubwa.

Kwa mujibu wa uchunguzi wake wa hospitali wa hivi karibuni, afya yake inaendelea kuimarika, na sasa anatarajia kurejea nyumbani.

"Kutokana na uchunguzi wa hospitali wa leo, hivi karibuni ninarudi nyumbani," alihitimisha.

Jose Chameleone alipelekwa Marekani kwa matibabu mwezi Januari 2025 baada ya hali yake kuwa mbaya, hali iliyowalazimu familia na marafiki zake kutafuta msaada wa haraka.

Awali, alilazwa katika hospitali moja jijini Kampala kabla ya kusafirishwa kwenda Boston kwa matibabu zaidi. Ugonjwa wake ulisababisha wasiwasi mkubwa kwa mashabiki wake, huku ripoti zikienea kuhusu hali yake kuwa mbaya.

Hata hivyo, sasa afya yake inaendelea kuimarika, na kurejea kwake Uganda kunatarajiwa kwa shauku kubwa. Mashabiki wake wanamsubiri kwa hamu kurejea kwenye jukwaa la muziki na kuendelea na kazi yake aliyoiendeleza kwa zaidi ya miongo miwili.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved