
ABBA Marcus, mwanawe msanii nguli wa muda mrefu kutoka Uganda, Jose Chameleone ameibuka tena na mashambulizi makali dhidi ya babake, saa chache baada ya taarifa za msanii huyo kutakiwa kufanyiwa matibabu ya kina kuibuka.
Kupitia ukurasa wa X, Marcus alifoka vikali alimlaani babake
na kumuita ‘Baba mbaya zaidi kuwahi kutokea katika historia ya dunia’ wakati
ambapo Chameleone anaelekea kufanyiwa upasuaji wa kongosho.
"I have the one of
the one of the worse father in the history of the world 😂" alichapisha, kabla ya kushiriki
machapisho kadhaa akielezea kufadhaika kwake.
Hii si mara ya kwanza kwa Marcus kumkosoa babake hadharani.
Matamshi yake ya hivi punde yanaonekana kutokana na kisa cha
hivi majuzi ambapo Chameleone alikimbizwa hospitalini lakini akachagua
kuzungumzia uvumi wa uongo kumhusu kwenye video ya moja kwa moja ya TikTok
kabla ya kuzungumza na watoto wake.
"Chameleone a ho... alikimbizwa hospitalini na jambo la kwanza
analofanya badala ya kuwasiliana na watoto wake, anaendesha TikTok live lol 😂😂😂"
alichapisha Marcus, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Chameleone na Daniella Atim.
Kijana huyo amekuwa akimshambulia babake mara kwa mara
kwenye mitandao ya kijamii, zaidi ya miezi miwili sasa tangu alipolazwa.
“Sifanyi hivi ili kufichua hulka za huyo mtu, ningeweza kuzembea kuanika
hovyo hovyo. Yeyote mwenye akili anajua yeye ni nani. Niko kwenye jukwaa LANGU
nikijieleza kwa sababu mtandao wa kijamii ni wa kujieleza,’ alijitetea
katika moja ya machapisho yake.