Msanii wa Kenya
Stephen Otieno Adera alimaarufu Stivo Simple boy alijiachillia aliposema kuwa kuwa yuko Single.
Alisema kuwa aliamua kuwa Kapera kutokana na sababu nyingi
za Wasichana kumtenda kinyume na mapenzi yake.
Alipozungumza akiwa katika mahojiano mnamo Ijumaa ya
Machi 21,2025, mzawa huyo wa Kibra aliweza kusema kuwa baada ya kupitia mapigo
kadhaa kimapenzi ya kukataliwa na wasichana
aliowapenda aliamua kupiga hatua kimaisha na sasa hataki uhusiano.
Msanii Stevo simple
boy anajulikana kutokana na ubunifu wake wa kuimba na kufanya mzaha kwa mashabiki wake
ambao amekuwa akiwawacha vinywa wazi .
‘’Nilipigwa matukio sasa niko Single ,Wanadada
walinikataa,sasa nikaamua mimi kama dragon,wacha tu niteme moto ‘’ Simple Boy alisema.
Maisha ya msanii stevo
simple boy yamechochea sana maisha ya wakenya akiwapendeza kama msanii
mchangamfu na mcheshi mkuu.
Ipo siku aliwahi kumtambulisha mrembo kwa jina Pritty Vishy
kama mrembo wake kabla ya wao kuachana kwa muda wa miezi michache.Hatimaye
aliweza kumtambulisha msichana mwingine kwa jina GRACE kama mchumba wake lakini
baadaye waliwachana tena.
Siku za hivi karibuni aliweza kupigwa na m shutuko baada ya
kukumbuka kuhusu zaidi ya mahusiano na wapenzi wake wa zamani ambapo
walimdanganya zaidi ya mara 10 Jambo lililomfanya abadili Mawazo na kusema
atafikiria masuala ya mapenzi mwaka wa 2026.
Simple boy aliweza kusema kuwa kuna vitu ambavyo yeye
huvichukia kama kukosa uaminifu katika uhusiano akikariri kuwa jambo hilo huweza
kuchangia pakubwa kuporomoka kwa mapenzi.
Stevo alisema kuwa aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Grace aliweza kuzalishwa na mwanamume
mwingine ilihali alikuwa na yeye bado katika mahusiano jambo ambalo lilimkata maini sana na kujihisi
mnyonge wa mapenzi na mtoro kwa sasa.
Alisema kuwa hata baada ya Grace kujifungua mwana
hakushughulika kutafuta babake mwana jambo ambalo lilimwacha akiwa amechanganyikiwa
na kumwacha katika hali tete.
‘’Tulikuwa sawa hapo mbele tulikuwa tunaishi vizuri mke
wangu alipokuwa karibu kujifungua mtu
alinipigia simu na akaninong’onezea kuwa alihitaji kuniambia jambo aliniambia
kuwa ulikuwa wakati mwafaka wa mimi kuambiwa ukweli na kuniambia kuwa nisikasirike,
aliniambia mtoto si wangu hilo jambo lilinicha na mawazo makubwa.