
SERIKALI ya Sudan imeendeleza mirindimo yake yak uikashifu serikali ya Kenya chini ya uongozi wake rais William Ruto baada ya kuwakubali wanamgambo wa kundi la RSF kukongamana Nairobi na kutia saini ya kuanzisha utawala mbadala jijini Khartoum.
Katika ujumbe wake mrefu kwenye X kupitia wizara ya masuala
ya kigeni, Sudan ilipongeza hatua ya baadhi ya mataifa kutoka ukanda wa Mashariki
ya Kati kupinga maelewano hayo yaliyotiwa saini jijini Nairobi siku chache
zilizopita.
Mataifa kama vile Qatar, Misri, Saudi Arabia miongoni mwa
mengine yamesimama kidete kutetea Sudani dhidi ya RSF na mikataba waliyotia
saini Nairobi wiki juzi.
“Wizara ya Mambo ya Nje
inafuata kwa shukrani na maslahi misimamo ya kimataifa iliyofuatana kukataa
tishio kwa mamlaka na umoja wa Sudan na uhalali wa kitaifa uliopo humo kupitia
jaribio la kuanzisha mamlaka kwa jina la wanamgambo wa Janjaweed na washirika
wake, kuanzia Kenya, na chini ya usimamizi wa mfadhili wa kikanda wa
wanamgambo.”
“Katika suala hili,
Wizara ilipongeza misimamo mikali ya kanuni iliyoonyeshwa na Jamhuri ya Kiarabu
ya Misri, Ufalme wa Saudi Arabia, Qatar, Kuwait, na nchi wanachama wa Baraza la
Usalama la Afrika: Algeria, Somalia, na Sierra Leone, na misimamo ya nchi
zingine wanachama wa Baraza: Urusi, Uchina, Amerika, Uingereza na Guyana, na
taarifa iliyotolewa na Türkiye,” wizara hiyo ilisema.
Katika kile kilichoonekana kama ni kufuma zaidi mkuki kwenye
moyo wa Kenya, Sudan iliikshifu Kenya ikisema kwamba kitendo chake kukubaslia
RSF jukwaa la kufanya shughuli zake za kutafuta amani jijini Nairobi ni sawa na
kuingia katika safu ya mataifa potovu duniani.
“Misimamo hii ya wazi
inathibitisha kwamba tabia ya kutowajibika ya rais wa Kenya, kwa kukumbatia
wanamgambo wa mauaji ya halaiki na kutaka kuhalalisha uhalifu wake ambao
haujawahi kushuhudiwa, imeitenga nje na ndani, na kuiweka Kenya katika kundi la
taifa potovu dhidi ya kanuni za kimataifa.”
Sudani iliendeleza Kauli za kutoa wito kwa jamii za kimataifa
na haswa muungano wa bara la Afrika kuingilia kati ili kukomesha kile ambacho
wanakiona kama ni ukiukaji mkubwa wa haki za kujitawala.
“Tunarudia wito wetu kwa
wanachama wote wa jumuiya ya kimataifa na mashirika ya kikanda na kimataifa, hasa
Umoja wa Afrika, kulaani tishio hili kubwa kwa amani na usalama wa kikanda na
kuharibu sheria zilizowekwa za mfumo wa kimataifa,” ujumbe huo uliotolewa
Jumatatu ulisema.