
Tume ya Umoja wa Mataifa juu ya Haki za Binadamu imesema viongozi wa Sudan Kusini wanahatarisha kurejea kwa mzozo ulioenea na kuvunjika kwa makubaliano dhaifu ya amani.
Taarifa hiyo iliyotolewa siku ya Ijumaa, iliangazia kuongezeka kwa mapigano katika Jimbo la Upper Nile na siasa za uchochezi katika mji mkuu, Juba.
"Haiwezekani kwamba miaka mingi baada ya uhuru wake, viongozi wa kisiasa bado wanaendeleza vurugu kote nchini, na kuwakatisha tamaa watu wa Sudani Kusini," alisema Yasmin Sooka, mwenyekiti wa tume hiyo.
Uchunguzi wa ripoti hiyo ulibaini kuwa mnamo mwaka 2024 mifumo ile ile ya ukiukwaji mkubwa katika maeneo yale yale, mara nyingi inahusisha ofisi zile zile za umma na za kijeshi.
Unyanyasaji wa kijinsia unaendelea katika maeneo ya ndani ya nje huku viongozi wakuu wakiendeleza mauaji, na kulazimisha wavulana kujisajili vitani na matukio ya kutekwa nyara huku wasichana wakiendelea kukabiliana na utumwa wa kijinsia, taarifa hiyo ilisema.
Yasmin Sooka alisema kuwa "Sudani Kusini inapaswa kusonga mbele, kutekeleza makubaliano ya amani, kuimarisha taasisi, na kujenga msingi wa demokrasia."
Sooka aliongeza kuwa cha kusikitisha ni kwamba,"Tunashuhudia hali ya kutisha ambayo inaweza kufuta maendeleo yaliyochukua miaka