logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mahakama yaamuru jogoo kuuawa kwa kuwapigia majirani kelele

Mwenye jogoo alisema alimnunua kwa ajili ya kumchinja Ijumaa.

image
na Radio Jambo

Michezo06 April 2023 - 07:13

Muhtasari


•Hakimu alimtaka  mwenye jogoo huyo kuhakikisha kwamba anamzuia kuzurura hadi Ijumaa atakapomchinja.

• Miaka kadhaa nyuma, mbuzi wa kiume alifikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa tuhuma za wizi wa kimabavu katika mahakama moja nchini humo.

Jogoo mwenye kero la kuwika kuchinjwa.

Visa vya wanyama kushtakiwa na kuhukumiwa adhabu mbalimbali si vigeni katika mahakama za mataifa mengi Afrika.

Nnchini Nigeria kwa mara nyingine tena, kesi ya jogoo mwenye kelele imezua gumzo mitandaoni baada ya kuhukumiwa kuuawa kisa kuwakera majirani kwa kelele.

 

Kulingana na jarida la AFP, jirani mmoja aliwasilisha kesi katika mahakama ya Jimbo la Kano, kaskazini mwa taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu, akilalamika jogoo wa jirani yake kukera kwa kelele za kuwika mara kwa mara.

Hakimu Halima Wali alitoa amri dhidi ya Malam Yusuf siku ya Jumanne akitangaza ndege huyo kuwa kero kwa jirani, kulingana na taratibu za mahakama zilizoonwa na AFP.

Yusuf aliambia mahakama kwamba alinunua ndege huyo ili kusherehekea Ijumaa Kuu na akaomba apewe hadi siku takatifu ya Kikristo kabla ya kumuua kwa ajili ya karamu ya familia.

Hakimu alikubali ombi hilo lakini akamuonya kuzuia jogoo huyo kuzurura eneo hilo na kuwasumbua wakaazi.

Pia alimtaka ahakikishe anamchinja ndege huyo siku ya Ijumaa kama alivyoahidi au atakabiliwa na adhabu kutoka kwa mahakama.

Si kinyume cha sheria kuweka mifugo na kuku katika nyumba katika sehemu kubwa ya Nigeria ambako wanafugwa kwa ajili ya chakula na kama mali ya pesa taslimu haraka katika dharura za kifedha.

Kesi kama hii katika eneo la kasikazini mwa Nigeria linalotawaliwa na idadi kubwa ya wumini wa Kiislamu iliripotiwa tena miaka kadhaa nyuma ambapo mbuzi wa kiume alifikwa mahakamani kwa tuhuma za wizi.

Katika taarifa hizo za kuchekesha na kuchanganya kwa wakati mmoja zilizochapishwa kwenye majarida mbalimbali ndani na nje ya taifa hilo, polisi washika doria walimpeleka mnyama huyo mwenye madoadoa meusi na meupe kwa polisi wakisema kuwa ni jambazi mwenye silaha ambaye alitumia uchawi kujigeuza mbuzi ili kukwepa kukamatwa baada ya kujaribu kuiba gari.

"Kikundi cha watu walinzi walikuja kuripoti kwamba walipokuwa kwenye doria waliona baadhi ya watu waliokuwa wakijaribu kuiba gari. Wakawafuata. Hata hivyo mmoja wao alitoroka huku mwingine akigeuka kuwa mbuzi,” jarida la Reuters lilinukuu taarifa za polisi wa Nigeria.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved