Aliyekuwa seneta wa Kakamega na mgombeaji wa kiti cha ugavana Kakamega mwakani 2017, Boniface Khalwale ameonyesha nia yake ya kuwania kiti hicho tena mwaka ujao.
Kupitia akaunyi yake ya Twitter, mwanasiasa huyo ambaye ni mwandani wa naibu rais William Ruto amekumbusha watu kuwa atakuwa akiwania kiti hicho kwa tikiti ya UDA.
Just a small reminder pic.twitter.com/K1o7tXI8WI
— Dr Boni Khalwale CBS, MBChB (@KBonimtetezi) May 22, 2021
Khalwale aliibuka wa pili baada ya kushindwa na Gavana Wycliffe Oparanya mwakani 2017. Atakuwa akitazamia kumridhi Oparanya baada ya kukamilisha mihula yake mbili inayoruhusiwa.