
Polisi wa kitengo cha ujasusi kutoka kituo cha Kutus kutoka kaunti ya Kirinyaga wamefanikiwa kumpata mtoto miezi 14 aliyekuwa ameripotiwa kupotea mnamo Januari 23, 2025.
Uchunguzi ulianzishwa wakati ambapo mamake mhusika aliandikisha ripoti katika kituo kimoja cha polisi huku akisimulia jinsi alivyopitia ugumu kutokana na kutoweka kwa mwanawe,alieleza kuwa alimuwacha mwanawe kwa jamaa yake akaenda kwa kinyozi kunyoa,wakati ambapo alirudi alighutushwa sana kupata kuwa jamaa yake na mwanawe hawakuwa wanaonekana tena.
Kwa kuhakikisha kuwa mwanawe anapatikana mzima tena buheri wa afya maafisa wa usalama walianzisha uchunguzi wa haraka ili kuhakikisha kuwa Maurine anapatikana pasi kukawia,walimtafuta kwa udi na uvumba ili wahakikishe kuwa mahali pale alipo anapatikana kwa kuangalia kamerakodi (CCTV) pamoja na kufuatilia kwa ukaribu deta za mtoro ili kubaini iwapo atanasika na kupatikana kwa wepesi.
Baada ya uchunguzi wa kina na wenye ufanisi mhusika aliyekuwa mafichoni hatimaye alipatikana akiwa amejificha eneo la Piai Katika gatuzi la Kirinyaga kufuatia operesheni kali iliyoendeshwa na makachero wa upelelezi wa DCI,Oparesheni hiyo iliyoendeshwa na hatimaye ikazaa matunda na mtoto akapatikana akiwa hai.
Hata hivyo uchunguzi ulivyokuwa ukiendelea Maurine ameonekana kuwa mwenye furaha na amefurahia kupatanishwa tena na mamake baada ya muda mrefu wa mahangaiko na kusononoka kila uchao.Kisa cha kutoweka kwa Maurine katika njia tatanishi kimewafumbua wazazi pamoja na walezi wengi macho kwa kuwa hawatazembea bali watakuwa makini na waangalifu wanapowaachia watu wa karibu au jamaa zao watoto.
Hata hivyo wakazi wa maeneo ya Kirinyaga wamevihongera sana vyombo vya usalama kwa kuwa macho na uaangalifu wa kupigiwa mfano kwa sababu kama hazingekuwa juhudi za maafisa wa usalama ingekuwa vigumu wao kumnusuru huyo mwana akiwa katika mikono ya mateka ambaye nia yake haijabainika wazi ni kwa nini aliazimia kufanya hivyo na kuwa mtoro.
Kisa hicho kikishuhudiwa wazazi wameshauriwa wawe makini na wasiwaamini watu tu kwa sababu ya kujuana kwa muda mfupi hasahasa wakaazi wanaoishi katika nyumba za kupanga ambao ujirani wao hauna mashiko wala arifa au maelezo mafupi kuhusu kila mmoja wao.