
Tigana Khalwale, mwanawe mwanasiasa na seneta wa Kakamega Boni Khalwale mnamo Jumanne usiku alinusurika kwenye ajali mbaya ya barabarani iliyotokea katika eneo la Ainabkoi, kaunti ya Uasin Gishu.
Seneta Boni Khalwale alifichua habari hizo Jumatano jioni kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii na kufichua kuwa mwanawe yuko salama.
Katika taarifa yake, seneta huyo alifichua kuwa Tigana hakujeruhiwa katika ajali hiyo na akamshukuru Mungu kwa kuokoa maisha ya mwanawe.
“Mwanangu, @TKhalwale, alitoka kwenye ajali hii katika eneo la Ainabkoi jana usiku akiwa hai na bila kujeruhiwa! Mungu ni mwema,” Khalwale alisema kupitia X.
Mwanasiasa huyo aliambatanisha taarifa yake na picha za gari la mwanawe ambalo lilikuwa limeharibiwa vibaya na ajali hiyo.
Wakenya kwenye mitandao ya kijamii walitoa maoni yao mbalimbali kuhusu ajali hiyo huku wengi wakionekana kufurahia kijana huyo kunusurika.
Tazama maoni ya baadhi ya Wakenya:
Martin: This was bad. God of second chances.
Samwel Wekesa: God is great. May He continue protecting your family.
Fabrice: May His name be praised.
Nene Wa Metha: That was close! But God is great he is safe.
Emoji: I pray he be well, and that’s God warning to you.