logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wazee wa Njuri Ncheke wanamtaka Waziri Muturi kurudi kwa Rais Ruto kutafuta suluhu.

Wazee wa Njuri Ncheke kutoka kaunti ya Meru sasa wanamtaka waziri wa utumishi wa umma Justine Muturi kuafikiana na rais William Ruto

image
na Japheth Nyongesa

Yanayojiri05 February 2025 - 11:50

Muhtasari


  • Hili limetokana na jitihada za waziri huyo kuikosoa serikali kutokana na misururu ya utekaji nyara ambao umekuwa ukiendelea nchini.
  • Wazee hao wamemutaka Muturi kuachana na mambo mengi ya vitina kwa serikali badala yake aendee kuchapa kazi kwa manufaa ya watu wa eneo hilo.

Kundi moja la wazee wa Njuri Ncheke kutoka kaunti ya Meru sasa wanamtaka waziri wa utumishi wa umma Justine Muturi kuafikiana na rais William Ruto kwa migogoro iliopo baina yao.

Hili limetokana na hatua ya waziri huyo kuikosoa serikali kutokana na misururu ya utekaji nyara ambao umekuwa ukiendelea nchini.

Wamesema kwamba iwapo wakati mwanawe alipotekwa nyara alimfikia rais na wakazungumza na yeye mbona asifanye hivyo jambo linapotokea ambalo si la kawaida katika taifa.

"Kama wazee wa Njuri Ncheke, tunakupenda Muturi, lakini tunakuomba, huwezi ukabomoa nyuma ukiwa ndani, rudi kwa mzee rais wako na Deputy Kithure Kindiki ndugu yako muongee. Kama kuna shida mahali maana wewe uko miongoni mwa wakubwa 22 ambao wanaweza kumfikia rais, kama ni ukweli unasema ulienda kuongea na rais si uende hata sasa uongee na yeye," mmoja wa wazee alisema.

Wazee hao wamemtaka Muturi kuachana na mambo mengi ya fitina kwa serikali badala yake aendelee kuchapa kazi kwa manufaa ya watu wa eneo hilo.

"Tunakuomba uwache hio fitina, rudi kwa serikali fanya kazi. Hatutaki siasa duni katika upande wetu ambao tunaita Mlima. Tunataka sisi tuwe kwa serikali tuwe tunaongea mambo ya serikali ndio tuweze kuendelea," wazee hao walendelea.

Kundi hilo limemtaka waziri Muturi kufatilia sheria za kazi na iwapo kuna jambo ambalo haliko sawa wamemtaka atafute mwafaka ili walizungumzie kwa kina.

"Embu, Meru, Tharaka sisi ni familia moja, na tunamtaka Muturi aungane na rais wetu kama ilivyokuwa pamoja na naibu wa rais. kama kuna jambo ambalo anaona haliendi sawa, tunamuomba waketi waongee walimalize ndio watu wetu wapate maendeleo," walisema wazee hao.


Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved