logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanawe Museveni Azindua Kura Ya Maoni, Awataka Waganda Kuamua Iwapo Besigye Asamehewe Au Anyongwe

Muhoozi ametishia kumnyonga kiongozi wa upinzani Kizza Besigye.

image
na Samuel Mainajournalist

Yanayojiri15 February 2025 - 12:21

Muhtasari


  • Muhoozi aliweka kura ya maoni  kwenye X ambapo aliwataka Waganda kupiga kura ikiwa wanataka Besigye  kunyongwa au kusamehewa.
  • Amewaomba raia wa Uganda kuendelea kupiga kura na akasema kuwa atafanya uamuzi Jumapili asubuhi.

Muhoozi Kainerugaba anataka Waganda kuamua ikiwa Kizza Besigye asamehewe au anyongwe

Muhoozi Kainerugaba, mwanawe Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni ambaye pia ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Uganda ametishia kumnyonga kiongozi wa upinzani Kizza Besigye.

Besigye amekuwa kizuizini tangu Novemba mwaka jana akikabiliana na mashtaka ya mahakama ya kijeshi. Kesi yake bado haijaamuliwa lakini Muhoozi ameendelea kudokeza kuwa inaweza kuisha kwa yeye kuchukuliwa hatua ya kunyongwa.

 Siku ya Jumamosi asubuhi, mwanawe rais Museveni aliweka kura ya maoni  kwenye Twitter ambapo aliwataka Waganda kupiga kura ikiwa wanataka kiongozi huyo wa upinzani kunyongwa au kusamehewa.

 “Wacha Waganda waamue hatima ya Besigye. Wanaotaka tumsamehe waretweet. Wanaomtaka anyongwe wa-like,” Muhoozi aliandika kwenye akaunti yake ya X.

Aliwaomba raia wa Uganda kuendelea kupiga kura na akasema kuwa atafanya uamuzi Jumapili asubuhi baada ya kuzungumza na Mungu na Yesu Kristo.

 Muhoozi alimtaja Besigye kama msaliti na akaweka wazi kuwa hatasita kumnyonga iwapo ataamua hivyo.

“Lakini nyote mnakumbuka. Besigye alitaka kumuua baba yangu. Miongoni mwa Bachwezi huo ni uhalifu mbaya zaidi! Lazima nimlinde baba yangu!!,” aliandika.

Haya yanajiri siku moja tu baada ya Besigye kufika katika Mahakama ya Hakimu Mkuu wa Buganda Road, akionekana dhaifu na mgonjwa, huku mifupa ya mabega yake ikilegea.

 Mashavu yake yaliyozama na macho matupu yaliashiria kuhusu siku ndefu bila kula chakula kinachofaa huku ngozi yake ikiwa nyembamba juu ya shavu lake maarufu.

 Macho yake yakiwa yanazunguka katika chumba cha mahakama, mtu aliweza kuona kwamba yalikuwa yakipepea kwa mchanganyiko wa wasiwasi na kutokuwa na uhakika.

 Mawakili wake wakiongozwa na Erias Lukwago waliambia mahakama kuwa kesi hiyo isiendelee.

 Alisema hali ya kiongozi huyo wa upinzani haitoi nafasi ya kuendelea na shughuli za siku hiyo, ni sawa na ukiukwaji wa haki zake za kibinadamu.

 Licha ya uamuzi wa Mahakama ya Juu kusitisha kesi za raia katika mahakama za kijeshi, Besigye bado yuko rumande akikabiliwa na mashtaka ya kijeshi.

 Rais wa Uganda Yoweri Museveni alisema serikali yake itaendelea kuwashtaki raia katika mahakama za kijeshi licha ya uamuzi wa Mahakama ya Juu.

 Besigye amekuwa rumande tangu Novemba 2024, alipozuiliwa baada ya kutekwa nyara jijini Nairobi.

 Alishtakiwa kwa kumiliki silaha kinyume cha sheria na usaliti, ambayo ina adhabu ya kifo.

 Pia anakabiliwa na mashtaka mengine.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved