logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wanajeshi wawili wa Uganda wakamatwa katika himaya ya Kenya

Kenya ilianzisha kikosi maalum cha ulinzi wa Pwani ili kushika doria katika maji ya Kenya na kuzuia muingilio wa vikosi vya nchi jirani na maharamia wengine.

image
na Davis Ojiambo

Hivi Punde05 February 2025 - 16:05

Muhtasari


  • Mbunge Raphael Wanjala alisema wanajeshi hao wa UPDF walikuwa na nia ya kuwasafirisha wavuvi hao hadi seli za kijeshi nchini Uganda ambapo mara nyingi wao huwadhalilisha, kuwadhulumu na kuwapiga.

Wanajeshi wa Uganda baada ya kutiwa nguvuni katika ziwa Victoria

Maafisa wa ulinzi wa Pwani nchini Kenya wamewatia mbaroni wanajeshi wawili wa Uganda katika ziwa Victoria.

Kulingana mbunge wa Budalang’i Raphael Wanjala wanajeshi hao wa Uganda walikuwa wameingia katika himaya ya Kenya na kuwakamata wavuvi raia wa Kenya karibu na kisiwa cha Sumba . Mbunge huyo alisema wanajeshi hao wa UPDF walikuwa na nia ya kuwasafirisha wavuvi hao hadi seli za kijeshi nchini Uganda ambapo mara nyingi wao huwadhalilisha, kuwadhulumu na kuwapiga.

“Maafisa wa Uganda ambao ni Konstebo Richard Amria na Michael Musila waliokuwa na bunduki aina ya AK 47 walikuwa tayari wamewakamata wavuvi wetu katika maji ya Kenya kwa nia ya kuwapeleka kwenye seli zao nchini Uganda kabla ya kikosi chetu cha Walinzi wa Pwani kuwakamata,” Wanjala alisema katika ujumbe wake kwenye mtandao wa Facebook.

Maafisa wa ulinzi wa Pwani wa Kenya kisha waliwapeleka wanajaeshi hao wa Uganda hadi kambi ya kijeshi ya Hakati na kuwakabidhi kwa idara ya jeshi la Kenya KDF ili washughulikiwe kuambatana na sheria.

Baadhi ya wananchi wanaoishi karibu na ziwa Victoria kaunti ya Busia walipongeza juhudi za maafisa wa ulinzi wa pwani huku wakisema kwamba wavuvi wakenya kwa muda mrefu wamekuwa wakihangaishwa na maafisa wa Uganda.

Kenya ilianzisha kikosi maalum cha ulinzi wa Pwani ili kushika doria katika maji ya Kenya na kuzuia muingilio wa vikosi vya nchi jirani na maharamia wengine.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved