
KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Februari 20.
Katika taarifa ya siku ya Jumatano jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti 11 za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Nairobi, Baringo, Nandi, West Pokot, Kakamega, Meru, Isiolo, Nyeri, Murang'a, Kiambu, na Taita Taveta.
Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za maeneo ya Gigiri, Sewage, Ruai, na Kilimani zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Mogotio na Kipsyenan katika kaunti za Nakuru na Baringo yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Eneo la Naramam katika kaunti ya West Pokot litaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za kaunti ya Nandi zikiwemo Kipture, Kipsigak, Kiminda, Kipsebwo na Kosoiywo pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Eneo la Harambe katika kaunti ya Kakamega litaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Katika kaunti ya Meru, sehemu za maeneo ya Ntugi, Kisima, na Marania zitakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Mutunyi, Kweruga, na Subuiga katika kaunti ya Isiolo yataathirika kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa tisa unusu alasiri.
Katika kaunti ya Nyeri, sehemu za Chinga na Muirungi zitakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi alasiri.
Maeneo ya Githunguri na Gaichanjiru katika kaunti ya Murang'a pia yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za maeneo ya Kikuyu na Magana katika kaunti ya Kiambu zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Manyani na Ndii katika kaunti ya Taita Taveta pia yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.