logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Sudan yasitisha ununuzi wa bidhaa kutoka Kenya

Taifa la Sudan siku ya Alhamisi Machi 13,2025 lilisitisha bidhaa zote zinazonunua kutoka taifa la Kenya.

image
na Evans Omoto

Yanayojiri14 March 2025 - 10:45

Muhtasari


  • Hatua hiyo ya Sudan ilifuatia baada ya kuishutumu Kenya kwa kuwa mwenyeji wa kundi haramu kutoka Sudan la RSF Alimaarufu (Rapid Support Force).‘
  • ’Bidhaa zote zilizokuwa zikinunuliwa kutoka taifa la Kenya kupitia bandari zote,vivukio,uwanja wa ndege  na viingilio vyote vimesitishwa kuanzia Machi 13,2025  hadi siku isiyo julikana’’.

Taifa la Sudan siku ya Alhamisi Machi 13,2025  lilisitisha bidhaa zote zinazonunua kutoka taifa la Kenya.

Hatua hiyo ya Sudan ilifuatia baada ya kuishutumu Kenya kwa kuwa mwenyeji wa kundi haramu kutoka Sudan la RSF Alimaarufu (Rapid Support Force).

‘’Bidhaa zote zilizokuwa zikinunuliwa kutoka taifa la Kenya kupitia bandari zote,vivukio,uwanja wa ndege  na viingilio vyote vimesitishwa kuanzia Machi 13,2025  hadi siku isiyo julikana’’.

Alisema kaimu msimamizi wa masuala ya biashara na usambazaji wa bidhaa Bwana  Ahmed Mohamed Ali.

Amri hiyo ilieleza kwa kuangazia maamuzi ya baraza la mawaziri kutoka kwa nambari 129 ya 2024  na pia kwa kuangazia nguvu zitokanazo na maamuzi ya baraza la magavana nambari 104 ya maka wa 2021.

Aidha maamuzi hayo pia yaliafikiwa kutoka kwa ripoti ya kamati ya baraza la magavana iliyoundwa kuanngazia hatua ya Kenya kuwa mwenyeji wa kundi la RSF hata hivyo iliafikiwa kuwa uamuzi huo uliangazia pia kulinda maslahi ya taifa la Sudan.

Mnano Februari  22,2025 Kundi la RSF  na baadhi ya makundi ya vyama vinavyo liunga mkono  waliweza kutia sahahi ya mkataba wa makubaliano katika jiji kuu la Nairobi Nchini Kenya wa kuwa na serikali mbadala katika himaya ya Sudan.

Siku mbili baadaye taifa la Sudan liliweza kuishutumu Kenya kwa kuunga mkono Kundi hilo haramu ambalo limekuwa likipinga  na kupigana na jeshi la Sudan SAF( Sudan Armed Forces)Tangu Aprili 2023.

Hivyo basi taifa la Sudan liliweza kutaja  hatua ya Kenya ya kualika na kuruhnusu mazungumzo hayo kufanyika katika himaya yake kama kitendo cha kuingilia usalama wa ndani wa taifa la Sudan  na kukiuka amri zote za  usalama  wa mataifa  ulimwenguni.

Katika taarifa yake Kenya kwa nchi ya  Sudan kupitia ubalozi  wa  Kenya uliweza kusema kuwa taifa la Kenya lilichukua maaamuzi hayo  kama njiamojawapo ya kuleta amani na upatanisho jambo ambalo liko katika Katiba yake.

Jeshi la Sudan limekuwa na mgogoro wa kivita na kundi la RSF tangu mwezi wa Aprili  2023 hadi mwisho wa mwaka wa 2024 mzozo huo uliosababisha vifo vya watu 29,683 kulingana na ripoti yaa kundi  moja la   takwimu za maganga.

Kulingana na ripoti ya waangalizi wa masuala ya uchumi inasemekana kuwa Sudan ndio nambari kumi kwa wingi wa kununua majani chai  kutoka Kenya  na nambari mbili katika bara la Afrika kwa ununuzi wa bidhaa hiyo.

Takwimu zilionyesha kuwa Taifa la Kenya liliuza dola milioni 48.2 za bidha zake katika taifa la Sudan  mwaka wa 2023.Kwa mauzo hayo bidhaa kubwa iliyouzwa  ilikuwa ni zao la majani chai dola milioni 29..6, Tumbaku  dola milioni 3.66 na zao la mbegu za mafuta dola milioni 1.84.

 Mauzo ya Bidhaa za Kenya katika taifa la Sudan yamepungua kwa kiwango cha asilimia 7.07 kwa miaka mitano iliyopita  ikipungua kutoka dola milioni 69.5 2018 hadi dola milioni 48.2 mwaka wa 2023.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved