
DCI waliwakamata washukiwa wawili wa ulanguzi wa dawa za kulevya na mihadarati.
Katika operesheni ambayo iliendeshwa dhidi ya kukomesha na kunasa dawa za
kulevya kama vile nikotini,usafirishaji na uuzaji wa dawa hizo.
Kikosi kizima cha kupambana na Mateja kwa ushirikianao na
maafisa wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Mugutha na maafisa wa
halimashauri ya polisi NGAO waliwakamata wasafirishaji wawili wa dawa hizo Pamoja
na misokoto ya bangi 800.
Mshukiwa wa Kwanza ambaye ana umri wa miaka 30, mwengine
wa miaka 21 walikamatwa wakiwa na misokoto hiyo katika mtaa wa Kimbo.
Maafisa hao hawakunasa tu misokoto bali waliweza kupata
hata bangi iliyokuwa katika Sacheti mbalimbali,Sacheti 13
zenye uzani wa giramu 35 kwa kila
moja ilihali sacheti tano zilikuwa na
uzani wa giramu 130 huku sacheti 44 zikiwa na uzani wa giramu 16 mtawalia.
Hata hivyo kuliwezwa
kunaswa mashine mawili ya kidigitali katika operesheni hiyo ambayo iliashiria
kuwa ilikuwa ni opereshini iliokuwa imepangwa kwa ustadi na kwa mtindo maalum.
Washukiwa hao wako katika kituo cha polisi ambapo uchunguzi wa kina unaendelezwa na maafisa wa polisi kuwahusu ipasavyo kabla ya wawili hao kufikishwa mahakamani.
Katika maeneo ya Moyale
mafisa wa kitengo cha kupiga doria waliweza kuikamata pikipiki yenye nambari ya usajili KMGM 369D ikiwa imebeba
magunia mawili yaliyoshukiwa kutokana na kile kilichokuwa ndani huku mwendeshaji
akitoroka na kuacha gari hilo barabarani.
Kwa kuweza kufanya msako na uchunguzi maafisa wa polisi
waliweza kupata ndani vifurushi 20 vya bangi ambapo ilikuwa na uzani wa kilo
100 ambapo pikipiki Pamoja na dawa hizo
ziko mikononi mwa polisi ambapo zimehifadhiwa kama Ushahidi.
Hata uchunguzi wa kina unaendelea ili kuweza kuwapata na
kuwakamata washukiwaa hao waliopatikana na dawa hizo amb po baada ya hapo wataweza
kushitakiwa kulingana na mjibu wa sheria.
Visa vya watu kupatikana wakisafirisha bangi na bidhaa za
magendo zimekuwa zikiripotiwa katika sehemu mbalimbali za jamuhuri ya Kenya huku wito kutoka kwa Idara
ya usalama ikizitaka taasisi za usalama kukaza mkono ili kuwakamata
wahusika.