

Matukio ya mvua kubwa ya pekee yanaweza kutokea katika baadhi ya maeneo ya Nyanda za Juu Mashariki na Magharibi mwa Bonde la Ufa, Bonde la Ziwa Victoria.
Sehemu zingine ambazo zinatarajiwa kupokea mvua ni Bonde la Ufa, nyanda za chini za Kusini-mashariki, Pwani, Kaskazini-mashariki na Kaskazini-magharibi mwa Kenya
Sehemu ambazo zinatarajia mvua kubwa ni pamoja na Nyanda za Juu Magharibi mwa Bonde la Ufa, Bonde la Ziwa Victoria.
Maeneo haya yanajumuisha kaunti zifuatazo(Siaya, Kisumu,Homabay, Migori, Kisii, Nyamira,Trans Nzoia, Baringo, Uasin Gishu,Elgeyo-Marakwet, Nandi, Nakuru, Narok, Kericho, Bomet, Kakamega, Vihiga, Bungoma, Busia na Pokot.
Kaskazini-magharibi (Turkana na Samburu] zitapokea mvua chache siku ya Jumamosi. Nyakati za asubuhi na usiku kutakua na kijibaridi kikali huku majira ya mchana yakishuhudia jua.
Kaskazini-mashariki (Marsabit,Mandera, Wajir, Garissa na Isiolo] Kaunti hizi zitapokea mvua ya mfululizo kwa siku tatu zijazo kuanza Ijumaa. Baadhi ya sehemu za kaunti hizo zitafunikwa na wingu zito na jua kwa asilimia chache mno.
Nyanda za chini za kusini-mashariki (Kitui, Makueni, Machakos, Kajiado na Kaunti za Taita Taveta na vile vile sehemu za bara za Kaunti ya Tana River.)
Sehemu hizi zitapokea mvua karibu maeneo yote siku ya Ijumaa, Jumamosi na Jumapili. Baadhi ya sehemu hizo mvua itaandamana na ngurumo za radi.
Maeneo ya Pwani (Mombasa, Kilifi, Lamu na Kaunti za Kwale pamoja na pwani sehemu za Mto Tana.) zitapokea mvua chache. Mvua ya rasharasha itashudiwa kwenye baadhi ya sehemu siku ya Jumamosi na Jumapili. Sehemu nyingi za maeneo hayo zitapokea joto la kadri kati ya nyusi 23'C - 36' C.