logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Basi la Super Metro lahusika katika ajali kwenye Barabara ya Thika

Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Jomoko, kati ya Witeithie na Thika, katika njia ya kushukisha abiria

image
na Samuel Mainajournalist

Yanayojiri29 March 2025 - 12:18

Muhtasari


  • Ajali ilihusisha basi la Super Metro na gari binafsi, ambapo basi hilo liligonga gari hilo kisha kupinduka barabarani, huku gari dogo likitumbukia mtaroni.
  • Ajali hiyo ilisababisha msongamano wa magari katika njia ya kushukisha abiria wakati shughuli za uokoaji zikiendelea.

Basi la Super Metro lilianguka Thika Road mnamo Machi 29, 2025.

Abiria waliokuwa ndani ya basi moja la kampuni ya Super Metro walinusurika bila majeraha baada ya ajali kutokea siku ya Jumamosi asubuhi kwenye Barabara ya Thika.

Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Jomoko, kati ya Witeithie na Thika, katika njia ya kushukisha abiria. 

Ilihusisha basi la Super Metro na gari binafsi, ambapo basi hilo liligonga gari hilo kisha kupinduka barabarani, huku gari dogo likitumbukia mtaroni.

Mashahidi na maafisa wa polisi waliripoti kuwa ingawa baadhi ya abiria walipatwa na mshtuko, hakuna aliyeripotiwa kujeruhiwa.

Video iliyosambaa mtandaoni ilionyesha wapita njia wakijitahidi kuwaokoa waliokuwa ndani ya basi hilo lililopinduka.

Ajali hiyo ilisababisha msongamano wa magari katika njia ya kushukisha abiria wakati shughuli za uokoaji zikiendelea.

Maafisa wa polisi wamethibitisha kuwa uchunguzi umeanzishwa ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Tukio hili linajiri wiki moja tu baada ya kampuni ya Super Metro kurejelea huduma zake kufuatia kusimamishwa kwa muda na Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama (NTSA).

Kampuni hiyo ya uchukuzi ilikuwa imesitishiwa shughuli zake mnamo Machi 20, 2025, kwa madai ya kutofuata kanuni za usalama.

Hata hivyo, mnamo Machi 24, Bodi ya Rufaa ya Leseni za Uchukuzi iliondoa marufuku hiyo, ikiruhusu kampuni hiyo kurejelea huduma zake mara moja.

Huku Super Metro ikiendelea kurejesha imani ya umma, ajali hii ya hivi punde imezua tena mjadala kuhusu usalama barabarani, hasa ikizingatiwa kuwa NTSA hapo awali ilikuwa na wasiwasi kuhusu ufuataji wa kanuni za usalama.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved