
Mshukiwa mmoja wa ulanguzi wa dawa za kulevya alikamatwa akiwa katika harakati za kusafirisha dawa hizo.
Maafisa wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Kamagambo waliweza kumkamata mshukiwa mmoja ambaye alipatikana na misokoto 401 ya bangi.
Kukamtwa kwa mshukiwa kulitokana na taarifa kutoka kwa wananchi wema ambao walikuwa macho sana na ambao walioonekana kumushuku mwanamume mshukiwa alipokuwa katika umati wa watu tayari kusafiri.
Baada ya raia kumshuku mshukiwa huyo waliweza kuwaarifu maafisa wa usalama kuhusu mienendo ya kutiliwa shaka kwa mshukiwa huyo pamoja na mizigo aliyokuwa amebeba.
Mshukiwa alikuwa tayari ameekwisha abiri gari aina ya Nisani nambari ya usajili KDM 981Z iliyokuwa ikisafiri kutoka Migoro ikielekea Kisumu ikiwa imebeba mizigo iliyoshukiwa ni haramu.
Maafisa wa polisi waliweza kuanzisha harakati za kulifuata gari hilo kwa upesi wa hali ya juu ili kulikamata na kuweza kulifanyia ukaguzi wa kupiga sachi, Katika kupiga sachi na kuweza kubaini kila na aina ya mizigo iliyokuwa imebebwa maafisa wa polisi waliweza kupata mikoba miwili iliyokuwa imebeba misokoto ya bangi 401,mzigo uiliyokuwa na uzani wa kilo 34.4 kulingana na taarifa ya DCI ambacho ni kiasi sawa na shilingi milioni moja na elfu thelathini 1.030M.
Katika pilikapilika za kufanya uchunguzi ndani ya gari hilo ilibainika kuwa mshukiwa mkuu wa gari hilo ambaye pia alikuwa ni Derva wa Gari hilo alikuwa amewabeba wanafunzi ambapo mshukiwa huyo alichukua fursa hiyo ya kutumia gari la abiria pamoja na wanafunzi kwa kisingizio kuwa hapo angeponyoka mtego wa polisi kwa haraka ila bahati yake ikaaambulia patupu.
Dereva wa Gari hilo alizuiliwa katika kituo cha polisi cha Kamagambo huku uchunguzi wa kina ukiendelea kuweza kubaini kiini cha tukio hilo huku baada ya uchunguzi wa kina kutamatishwa Dereva ataweza kufikishwa mahakamanio ili kujibu mashitaka ya kutumia gari la umma kusafirishia mizigo haramu miongoni kwa mashitaka mengine ambayo atapatikana nayo.
Maafisa wa usalama waliendelea kuwaomba wananchi kuwa macho kila wakati waonapo matukio yasio sahihi na kufanya jitihada za kuripoti matujkio hayo kwa haraka iwezekanavyo kwa kupiga simu kwa nambari 0800722203 ya fichua siri usiogope bila malipo yoyote.