
Shirika la kusambaza umeme nchini la Kenya Power (KPLC) limetangaza kuwa huduma ya umeme itakatizwa kwa muda katika maeneo mbalimbali ya kaunti sita Jumanne, Aprili 15, 2025.
Katika taarifa rasmi, kampuni hiyo imesema kuwa kukatika kwa umeme kutasaidia kuruhusu matengenezo ya mfumo wa usambazaji pamoja na uboreshaji wa miundombinu.
Umeme utakatika kwa nyakati tofauti kati ya saa mbili asubuhi hadi saa kumi na moja jioni. Kaunti zitakazoathirika ni Nairobi, Uasin Gishu, Kisumu, Homa Bay, Murang’a na Mombasa.
Nairobi
Maeneo yatakayokosa umeme kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni ni:
- Kanisa la King of Judah
- Chuo cha Urembo cha Bimz
- Swaminarayan Academy
- Sehemu ya Githurai 44
- Sehemu ya Zimmerman na vitongoji vyake
Uasin Gishu
Katika kaunti ya Uasin Gishu, umeme utakatika kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na moja jioni katika maeneo yafuatayo:
- Mugunga
- Sipande
- Mlimani
- Pan Paper
- Luanda Lugari
- Munge
- KMTC
- Mbogo
- Langas Corner
- Ndupawa
- Relax Inn
- Jijenge Quarry
- Hoteli ya Starbucks na maeneo jirani
Kisumu
Umeme utakatika kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa tisa alasiri katika:
- Sondu
- Nyabondo
- Chebera
- Shule ya Wasichana ya Nyakach
Homa Bay
Maeneo ya Homa Bay yatakosa umeme kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi jioni, yakiwemo:
- Soko la Kendubay
- Shule ya Msingi ya Ayub Akoko
- Soko la Kanyandhiang
- Shule ya Upili ya Nyangacho
- Masoko ya Dago, Oriang, Adiedo, na Pala
- Homahills
- Hospitali na Shule ya Upili ya Gendia
- Gereza la Homabay
Murang’a
Maeneo yatakayoathirika kuanzia saa
tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni ni:
- Hospitali ya Maragwa Level 5
- Zahanati ya Kamung’ang’a
- Kiwanda cha Equitorial Nut Processors
- Afrimac
- Shule ya Pioneer
- Shule ya Upili ya Muthithi
- Masoko ya Kaharati na Igikiro
- Mji wa Maragua
- Bishop Mahiani Academy
- Shule ya Wavulana ya Igikiro
- Shamba la Mhote
- Shule ya Viziwi ya Murang’a
- Maragwa Ridge, Gachocho, Kahariro na vitongoji vya
karibu
Mombasa
Mombasa pia itakumbwa na kukatika kwa umeme kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni, hususan maeneo yafuatayo:
- Wayani
- Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mombasa
- Lecol
- Sehemu ya Kituo cha Polisi cha Mbaraki
- Mbaraki Sports Club
- Petro Likoni
- Hoteli ya Shenai
- Hospitali ya Aga Khan
- Sehemu ya Kizingo na maeneo ya karibu