
Shirika la Kenya Power limetangaza kuwa kutakuwa na kukatika kwa umeme katika kaunti sita Alhamisi hii, kufuatia matengenezo ya kawaida na uboreshaji wa mifumo.
Kaunti zitakazoathirika ni Nairobi, Kisii, Kiambu, Kilifi, Kirinyaga, na Embu. Umeme utakatika kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 11 jioni katika maeneo mengi.
Katika Kaunti ya Nairobi, sehemu za Pangani zitakuwa bila umeme. Maeneo yatakayoathirika ni Barabara ya Marang’a, Hospitali ya Guru Nanak, Kituo cha Polisi cha Pangani, Barabara ya Juja, Hospitali ya Radiant, Shule ya Wasichana ya Pangani, Hospitali ya Alamin, Makao Makuu ya KICD, na sehemu za Barabara za Muratina na Fair View pamoja na maeneo jirani.
Katika Kaunti ya Kisii, maeneo ya Nyamache, Igare, na Kiobegi yataathirika. Taasisi zitakazokumbwa ni Kiwanda cha Chai cha Nyamache, Soko la Emenwa, Shule ya Upili ya Matierio, Soko la Igare, Shule za Wasichana na Wavulana za Nyamagwa, Shule ya Boitangare, Matierio Keigamere, na Shule ya Upili ya Kionduso.
Katika Kaunti ya Kirinyaga, umeme utakatika katika sehemu za Mji wa Kagio na maeneo jirani kama Kiunga, Mitarabo, Kandongu, Chuo cha Ufundi cha Kiamachiri, Shule ya Wasichana ya Mutithi, na Shule ya Msingi ya Gitooni.
Katika Kaunti ya Embu, maeneo ya Gatondo na Maramuri yatakosa umeme. Taasisi zitakazoathirika ni Gatondo, Havard, Shule ya Upili ya Embu, Kamutungi, Muiganania, na sehemu za Muthatari.
Kaunti ya Kiambu itashuhudia kukatika kwa umeme katika eneo la Kamiti na maeneo yanayozunguka. Maeneo hayo ni pamoja na Kambi ya Ngethu, Soko la Ngorongo, Kariua, Kamwangi, Hospitali ya Igegania, Kairi, Nyamagara, Kangoo, Mukurwe, Gatei, Kanjuku, Watathi, Gathaite, Mbici, Ruburi, Mbogoro, Kimee, Kagumoini, Ritho, Icaciri, Gitatiini, Ituiku na Gitundu.
Katika Kaunti ya Kilifi,
sehemu za Kokotoni, Kanamai na Mtwapa zitakumbwa na kukatika kwa umeme.
Biashara na taasisi zitakazoathirika ni Iron Africa, Kavee Quarry, SS Mehta,
Miritini Products Ltd, Kijiji cha Wasomali, Greenwood, Coca-Cola Bottlers,
Milly Fruits, Mzuri Sweets, Umoja Rubber, Chuo cha Afya cha Northcoast, na
maeneo mbalimbali ya Bomani, Junju, na Mwatundo.
Kenya Power imewataka wakazi wa maeneo yaliyoathiriwa kuchukua tahadhari na kupanga shughuli zao ipasavyo.