
REAL MADRID wanafikiria KUACHANA na LaLiga, kwa mujibu wa ripoti za hivi majuzi.
Miamba hao wa Uhispania kwa sasa wako kileleni mwa jedwali, alama sawa na Barcelona japo kwa uchache wa mabao na wako mbioni kutwaa ubingwa.
Lakini Real Madrid wanazozana na rais wa LaLiga Javier Tebas
na bodi ya waamuzi.
Kutoridhika kwa klabu hiyo kumekuja baada ya kukithiri kwa
dhuluma uwanjani katika michezo ya hivi majuzi.
Hizi ni pamoja na kukosa kadi nyekundu kwa mpinzani Carlos
Romero kwa kumchezea rafu Kylian Mbappe katika kipigo cha 1-0 kutoka kwa
Espanyol. Romero aliishia kufunga bao la ushindi katika mechi hiyo.
Klabu hiyo ilijibu tukio hilo kwa kauli yenye maneno makali,
ambayo ilimfanya Tebas kudai "wamerukwa na akili".
Pia kulikuwa na malalamiko juu ya kadi nyekundu ya Jude
Bellingham dhidi ya Osasuna wikendi.
Carlo Ancelotti alijibu kwamba "VAR lazima iwe
imezimwa" huku kiungo huyo akikabiliwa na KUPIGWA MARUFUKU YA MECHI 12.
Waamuzi wa LaLiga wameonyesha kuwa wako tayari kugoma baada
ya Real Madrid kudai kuwa maamuzi yao yalikuwa "yakichezewa".
Katika mabadiliko ya hivi punde, jarida la Uhispania la
SPORT limedai kuwa klabu hiyo sasa inatafuta "kimbilio" kutoka kwa LaLiga
na kuhamia ligi ya kigeni.
Ili kufanya mabadiliko hayo kuwa ukweli rais wa klabu
Florentino Perez angehitaji kupata kibali kutoka Fifa.
Angelazimika kuomba mabadiliko ya ushindani ambayo pia
yangehitaji ‘ndio’ kutoka LaLiga.
Hii itafuatwa na kuomba ruhusa kutoka Uefa - shirika ambalo
Real Madrid walitaka kuondoka ili kuunda Ligi Kuu ya Uropa.
Ripoti hiyo pia imedai kuwa Real Madrid inaamini kwamba
Tebas amezishawishi vilabu vingine kwenye ligi dhidi yao kwenye
"msalaba" dhidi ya Madrid.
Jarida la Forbes limedokeza kwamba vivutio vya Real Madrid
vitakuwa ligi za Ufaransa, Ujerumani na Italia.
Haiwezekani kwamba Ligi ya Premia itazingatiwa baada ya
klabu hiyo kusikika kuhamia Uingereza katika miaka ya nyuma.