
KOCHA wa Chelsea, Enzo Maresca amewajibu baadhi ya wachambuzi wa soka wanaomkosoa kwa kumchezesha nahodha Reece James kiungo cha kati badala ya beki wa kulia.
Kwa mujibu wa Muitaliano huyo, uamuzi wa kumchezesha Reece
James katika kiungo cha kiungo ni sehemu ya mpango wa kumlinda dhidi ya
majeraha.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 amehusika katika
michezo yote isipokuwa miwili kati ya 11 iliyopita na anazidi kucheza katika
safu ya kiungo.
Hata hivyo, meneja wake wa zamani Thomas Tuchel alisema
anapendelea nahodha wa klabu ya Chelsea katika nafasi ya beki wa kulia huku
mlinzi wa zamani John Terry akirejea maneno yake katika mahojiano na BBC Sport.
Hata hivyo, Maresca anasema kuwa nafasi ya kiungo ni sehemu
ya mkakati mpana zaidi wa kumbakisha uwanjani James, ambaye amekuwa na majeruhi
15 ndani ya misimu mitano.
“Kwa upande wa data
unaona beki wa pembeni anapocheza kwa jinsi alivyokuwa akicheza, kupanda na
kushuka (hufanya hivyo) sana, sana, mara nyingi zaidi (mara nyingi) kuliko
kuingia ndani kwa umbali (mkubwa zaidi), kwa muda wa kupanda na kushuka,” alisema.
Alisisitiza kwamba ataendelea kumchezesha Reece James katika
sehemu tofauti tofauti bila kujali ukosoaji kutoka kwa wachambuzi wa soka.
"Mwaka jana huko Leicester tulikuwa na Ricardo Pereira,
kwamba anaweza kuwa mchezaji wa juu kwa timu ya juu, lakini kwa sababu ya
majeraha yake ... mwaka jana na sisi alicheza michezo yote, tulibadilika kidogo
na hiyo inafanya kazi vizuri.
"Nikiwa na James,
inafanya kazi vizuri. Lakini tayari nilisema mara nyingi, Reece pamoja nasi
anacheza beki wa kulia, beki wa kushoto, kiungo - nafasi tofauti.”
"Siyo peke yake.
Tuna wachezaji wengi zaidi wanaocheza katika nafasi tofauti. Kwa hivyo tuna
furaha na tunatumai jinsi tunavyomtumia Reece inamsaidia kuwa fiti."
Maresca pia alisema kuwa James bado hawezi kuanza mechi kila
baada ya siku tatu na anasimamiwa kwa uangalifu mkubwa na kuongeza:
"Tunajaribu kila siku kuwa na wahudumu wa afya
wazungumze naye kuona yukoje, ikiwa ana uwezo wa kufanya mazoezi, akiwa mzuri,
kama sio mzuri.
"Kusema kweli, katika wiki za hivi karibuni amekuwa
akifanya mazoezi kila siku. Hii ndiyo sababu tunafurahishwa na hilo na hatutaki
alazimishe na apate shida nyingine.