logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Gwiji wa Marathon Mary Keitany astaafu kufuatia jeraha

Keitany amestaafu akiwa amenyakua mataji matatu ya mbio za London Marathon, mataji manne ya mbio za New York Marathon, na mataji mawili ya World Half Marathon

image
na Radio Jambo

Makala23 September 2021 - 06:54

Muhtasari


•Keitany amestaafu akiwa amenyakua mataji matatu ya mbio za London Marathon, mataji manne ya mbio za New York Marathon, na mataji mawili ya World Half Marathon

Mwanariadha Mary Keitany ametangaza kustaafu kwake kutokana na maumivu ya mgongo.

Keitany ambaye amekuwa kwenye ulingo wa riadha kwa zaidi ya miaka kumi alitangaza kustaafu kwake siku ya Jumatano akiwa na umri wa miaka 39.

Mwanariadha huyo ambaye anashikilia rekodi ya mbio za Marathon za wanawake pekee alisema kuwa jeraha ambalo alipata mwaka wa 2019 ndilo limesababisha uamuzi huo.

"Kila nilipoona kana kwamba nimepata nafuu kabisa na kuanza kufanya mazoezi jeraha lile lilikuwa linaanza kusumbua tena. Sasa ni wakati wa kusema kwaheri kwa mchezo ninaoupenda sana" Keitany aliambia wanahabari.

Keitany amestaafu akiwa amenyakua mataji matatu ya mbio za London Marathon, mataji manne ya mbio za New York Marathon, na mataji mawili ya World Half Marathon.

Keitany aliumia mwaka wa 2019 alipokuwa anashiriki katika mbio za London Marathon na hajaweza kufanya mazoezi vizuri tangu wakati huo.

"Safari kubwa ambayo imeisha. Najivunia yale nimefanya na nawashukuru kwa kuniunga mkono kutoka kote ulimwenguni. Ukurasa mwingine wa maisha yangu unaanza" Keitany aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved