Hatua
ya Makundi ya Mashindano ya Ligi ya Mabingwa ilikamilika usiku wa Jumatano,
Januari 29 huku mashabiki wakifurahia michuano 18 iliyoanza kwa wakati mmoja
kote Ulaya.
Wahitimu wa hatua ya muondoano walithibitishwa huku timu 24 zikisonga mbele kwa awamu inayofuata ya mashindano hayo ya kifahari ya Uropa.
Kati ya hizo 24, timu nane zilifuzu moja kwa moja kwenye hatua ya 16 bora huku timu 16 zilizosalia zitacheza hatua ya muondoano kwa mikondo miwili ili kusonga mbele.
Timu 12 zilizomaliza katika nafasi za mwisho ziliondolewa kwenye mashindano na hivyo kuhitimisha kampeni zao za Uropa.
Tazama jedwali la mwisho la hatua ya makundi hapa chini.
1. Liverpool (moja kwa moja kutinga hatua ya 16 bora)
2. Barcelona (moja kwa moja kutinga hatua ya 16 bora)
3. Arsenal (moja kwa moja kutinga hatua ya 16 bora)
4. Inter (moja kwa moja hadi 16 bora)
5. Atletico Madrid (moja kwa moja hadi 16 bora)
6. Bayer Leverkusen (moja kwa moja hadi 16 bora)
7. Lille (moja kwa moja hadi 16 bora)
8. Aston Villa (moja kwa moja hadi 16 bora)
9. Atalanta ((raundi ya muondoano kuingia hatua ya 16 bora))
10. Borussia Dortmund ((raundi ya muondoano kuingia hatua ya 16 bora))
11. Real Madrid (raundi ya muondoano kuingia hatua ya 16 bora)
12. Bayern ((raundi ya muondoano kuingia hatua ya 16 bora))
13. AC Milan (raundi ya muondoano kuingia hatua ya 16 bora)
14. PSV (raundi ya muondoano kuingia hatua ya 16 bora)
15. PSG (raundi ya muondoano kuingia hatua ya 16 bora)
16. Benfica (raundi ya muondoano kuingia hatua ya 16 bora)
17. Monaco (raundi ya muondoano kuingia hatua ya 16 bora)
18. Brest (raundi ya muondoano kuingia hatua ya 16 bora)
19. Feyenoord (raundi ya muondoano kuingia hatua ya 16 bora))
20. Juventus (raundi ya muondoano kuingia hatua ya 16 bora)
21. Celtic (raundi ya muondoano kuingia hatua ya 16 bora)
22. Man City (raundi ya muondoano kuingia hatua ya 16 bora)
23. Sporting Lisbon(raundi ya muondoano kuingia hatua ya 16 bora)
24. Club Brugge (raundi ya muondoano kuingia hatua ya 16 bora)
25. Dinamo Zagreb (Waliondolewa)
26. Stuttgart (Waliondolewa)
27. Shakhtar Donetsk (Waliondolewa)
28. Bologna (Waliondolewa)
29. Crvenza Zvezda (Waliondolewa)
30. Sturm Graz (Waliondolewa)
31. Sparta Praha (Waliondolewa)
32. RB Leipzig (Waliondolewa)
33. Girona (Waliondolewa)
34. RB Salzburg (Waliondolewa)
35. Slovan (Waliondolewa)
36.
Young Boys (waliondolewa)
Mashindano hayo ya kifahari ya Uropa yatakamilika kwa fainali itakayochezwa Jumamosi, 31 Mei, kwenye Uwanja wa Allianz Arena huko Bayern Munich.