logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Rais wa FKF Hussein Mohammed akanusha madai kwamba tiketi zote ziliuzwa Kenya ikichuana na Gabon

Hussein Mohammed amekanusha madai ya hapo awali kwamba tiketi zote za kutizama mpira ziliuzwa.

image
na Japheth Nyongesa

Football25 March 2025 - 16:33

Muhtasari


  • "Nafikiria ni jambo la muhimu tuelewe uwezo wa kukaa katika uwanja huo, nimeona mambo mengi yakisambaa. Nadhani viti vyote kwa pamoja katika uwannja ni 22 000. Hiyo ndiyo tarifa ambayo tuko nayo kutoka kwa wasimamizi wa viwanja. Viti vya watu wa kawaida ni karibia 18, 000, kisha 4000 kwa wageni mashuhuri 'VIP',' aliweka wazi.

Harambee Stars supporters watching football at Nyayo Stadium while Kenya Playing against Gabon

Rais wa shirikisho la soka nchini FKF Hussein Mohammed amekanusha madai ya hapo awali kwamba tiketi zote za kutizama mpira kati ya timu ya taifa Harambee Stars na Gabon zilikuwa zimeuzwa zote.

Wakati akizungumza kwenye kikao na wanahabari pia alitupilia mbali fununu za awali kwamba uwanjwa wa kimataifa wa Nyayo una uwezo wa kustahimili mashabiki wapatao 30, 000.

Mohammed alifichua kwamba uwanja huo ambao umeidhinishwa na CAF hivi karibuni umeundwa na uwezo wa kuhifadhi mashabiki elifu 22,000.

"Nafikiria ni jambo la muhimu tuelewe uwezo wa kukaa katika uwanja huo, nimeona mambo mengi yakisambaa. Nadhani viti vyote kwa pamoja katika uwannja ni 22 000. Hiyo ndiyo taarifa ambayo tuko nayo kutoka kwa wasimamizi wa viwanja. Viti vya watu wa kawaida ni karibia 18, 000, kisha 4000 kwa wageni mashuhuri 'VIP',' aliweka wazi.

Rais wa shirikisho pia alieleza kwamba hawakutakiwa kuuza tiketi zote kwa sababu ya changamoto ambazo huambatana na michezo. Akitaja kuvunjika kwa malango ya kuingiwa uwanjani ambayo yalisababisha mashabiki wengine kuingia uwanjani kama changamoto ambazo hutarajiwa.

'Haikuwa tuuze asilimia 100% ya tiketi, tuliuza chini kidogo. Kwa ajili ya kuweka uwazi, watu wa kawaida tuliuza tiketi 15, 968, VIP 1331, VVIP 107. Tuliacha kuuza tiketi tulipofikia hapo. Kwa mfano Gate namba 2 na 8 zilivunjika na watu wakaingia," alieleza.

"Kulikuweko na magari ambayo yalipakiwa na yalikuwa 329. tiketi zote ambazo zilliuzwa kwa pamoja zilikuwa 17 130 siku ya Jumapili," alisema.

Uwanja wa Nyayo umetumika na timu ya Harambee stars kwa mara ya kwanza baada ya kukarabatiwa kwa zaidi ya miaka minne.

Uwanja huyo ni mojawapo ya viwanja ambavyo vinatarajiwa kutumika wakati Kenya itakapokuwa mwenyeji wa CHAN na AFCON mwaka huu na mwaka 2027 mtawalia. Kenya itaandaa mashindano haya kwa kushiriani na Uganda pamoja na Tanzania.

Harambee Stars ilipoteza nyumbani baada ya kupigwa na wageni Gabon mabao mawili kwa Moja. Bao la Kenya likifungwa na nahodha Michael Olunga.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved