logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Kwaheri mama!" Mtangazaji Ghost Mulee aomboleza mtu wa karibu

Ghost anaomboleza kifo cha mtu aliyekuwa na nafasi kubwa maishani mwake.

image
na Samuel Mainajournalist

Vipindi26 March 2025 - 14:45

Muhtasari


  • Ghost alifafanua kuwa marehemu alikuwa mama wa rafiki yake mkubwa, lakini kwa karibu miaka 30, amemchukulia kama mzazi wake.
  • Ghost alisimulia mkutano wake wa mwisho na mama huyo ajuza, aliyekuwa akielekea kutimiza miaka 94.

Jacob 'Ghost' Mulee

Jacob ‘Ghost’ Mulee, mtangazaji mwenza wa kipindi cha Gidi na Ghost Asubuhi kwenye Radio Jambo, anaomboleza kifo cha mtu aliyekuwa na nafasi kubwa maishani mwake.

Siku ya Jumatano alasiri, kocha huyo wa zamani wa Harambee Stars alichapisha video akielekea kwenye mazishi ya mwanamke aliyemchukulia kama mama yake.

Katika video hiyo, alifafanua kuwa marehemu alikuwa mama wa rafiki yake mkubwa, lakini kwa karibu miaka 30, amemchukulia kama mzazi wake.

“Hii ni siku ya huzuni kwa sababu naenda kumzika mama yangu. Ni mama yangu kwa kweli, kwani ni mama wa rafiki yangu, Bw. Munaa Kalaiya. Tumemchukulia kama mama yetu kwa miaka mingi tangu nilipokutana na Munaa zaidi ya miaka 30 iliyopita,” alisema.

Mtangazaji huyo mcheshi wa kipindi cha asubuhi pia alisimulia mkutano wake wa mwisho na mama huyo ajuza, aliyekuwa akielekea kutimiza miaka 94.

Ghost alifichua kuwa alipata fursa ya kupokea baraka zake mapema mwezi huu wakati walipomtembelea nyumbani kwake.

“Majuma mawili yaliyopita tulipata nafasi ya kusherehekea maisha yake. Alikuwa ametimiza miaka 93 na alitarajiwa kusherehekea miaka 94 ifikapo Aprili. Tulimtembelea kama kawaida kwa ajili ya baraka na msamaha. Inatia faraja kujua kwamba sasa amepumzika akiwa na miaka 93,” aliongeza.

Alihitimisha kwa ujumbe wa kugusa moyo kwa familia ya marehemu, akisema: “Ninataka tu kusema, Mungu aiweke roho yake mahali pema. Kwa familia ya Munaa, poleni kwa sababu huu ni mwendo wa kila mmoja wetu. Pumzika kwa amani, Mama Munaa.”

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved