
Jamaa aliyejitambulisha kama Hosea Baraza ,25, kutoka Bungoma alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Emily Nelima ,23, ambaye alitoroka nyumbani.
Hosea alisema ndoa yake ya mwaka mmoja na miezi tatu ilianza kuyumba wakati mk wake alianza kuongea na mwanaume mwingine.
Alisema mkewe aliondoka baada ya kuzozana na akabeba vitu za nyumba.
"Ilifika mahali akifika kwa nyumba anaweka simu yake katika flight mode. Siku nyingine nikaichukua, kuna jumbe ziliingia kwa simu yake. Nilipomuuliza akakasirika. Kulikuwa na jamaa alikuwa anaongea na yeye. Ata kuna wakati nilitaka nimuulize huyo jamaa kwa nini anaongea na bibi yangu na ako na familia yake. Lakini niliacha ," Hosea alisimulia.
"Sielewi mahali ako saai. Nikipiga simu sasa hawezi shika. Huyo jamaa ni mwalimu alikuwa anafunza shule ya pili. Namjua, wametoka pande moja. Huenda ameenda kwa mwalimu huko mombasa.Sikuwa nimepeleka mahari, tulikuwa tunaishi na yeye kama mke wangu," aliongeza.
Juhudi za kumpatanisha Hosea na mkewe hata hivyo ziligonga mwamba kwani Emily hakushika simu yake alipopigiwa.
Hosea alisema kwa uchungu, "Ni kama anajua kitu inaendelea kwa sababu. Mtu kuita mke wako babe inauma sana. Mke ambaye unalisha. Na ni mtu ambaye ako na familia. Huyo jamaa aliikuwa anamwambia anataka kumtafutia kazi na kumeweka mahali pengine pazuri."
"Alinibebea vitu. Hakubeba zote. Alichukua vitu zangu za kazi, woofer, gas cooker, nguo zake. Aliacha t-shirts kama tatu ambazo havai. Nilikuwa nafanya kila kitu. Yeye pia ni hardworking, tukiondoka kwa nyumba tulikuwa tunapatana jioni," aliongeza.
Alipoulizwa ikiwa alikuwa amemuoa Emily rasmi, na uthibitisho wa hilo, Hosea alisema, "Kuna zile maselfie ambazo tulikuwa tunapiga kwa nyumba, niko na ID yake, kuna vitu mingi ambazo niko nazo ambazo siwezi kuzungumzia. Ni mtu ambaye tumekaa na yeye muda mrefu. Ata watu wa kwao wanajua, mandugu zake wanajua."
Katika maneno yake ya mwisho kwa mpenziwe, Hosea alisema, "Mimi sikuwa na ubaya na wewe. Nilikuwa nakupenda sana, nilikuwa nakuheshimu. Sikutaka maisha yako na yangu itengane juu ya watu wa nje. Kama uliamua hivyo ni sawa huenda tukakutana, sina ubaya na wewe.