logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: Jamaa adai mkewe ako na mimba ya miezi 3, mke asema hafahamu ni mjamzito

"Kuna siku nilikwambia niko na mimba? Mimi niwe na mimba na sijui? Kuna siku umenipeleka kliniki? Sina mimba!" Anita alisema.

image
na Samuel Mainajournalist

Patanisho03 February 2025 - 08:38

Muhtasari


  • Victor alisema ndoa yake ya miaka mitatu ilisambaratika siku nne zilizopita wakati mkewe alipotoroka kufuatia mzozo wa kinyumbani.
  • "Nikimwambia anipeleke kwao, ananiambia nijipange nimpeleke kwetu. Kati yangu na yeye, nani ameoa mwingine," Anita alisema.

Victor Kiza mwenye umri wa miaka 35 kutoka Embakasi alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Anita Magomere (35) ambaye alikosana na mke wake hivi majuzi.

Victor alisema ndoa yake ya miaka mitatu ilisambaratika siku nne zilizopita wakati mkewe alipotoroka kufuatia mzozo wa kinyumbani.

"Nimemuoa kwa miaka 3. Tumekuwa tukisumbuana, anaenda akirudi. Ako na mimba ya miezi tatu. Kuna siku tumekosana hapo. Nikaenda kazini, kurudi nikapata amebeba vitu zake akaenda. Kumpigia simu vile aliniongelesha labda nikuje Patanisho," Victor alisema.

Alieleza kwamba amesononeka sana baada ya mkewe kuondoka.

"Nyumba haikaliki baada ya yeye kuenda, nahisi kuna kitu kubwa kinakosa. Kumpiga ninakubali nilimpiga kwa sababu ya mabishano kwa nyumba. Nikawa na hasira nikampiga. Sasa hivi najuta, niko na upweke. Nitaanzia wapi na nimezoea kuna mtu ananipikia. Nampigia simu hashiki. Nilijaribu kuongea na watu wa kwao nikaona ni kama wanaegemea upande wake," alisema.

Anita alipopigiwa simu na kuelezwa jinsi mumewe alivyosononeka kwa kumkosa nyumbani, alisema, "Kwa nini hakuli? Huyo anaweza kosa kukula?"

Alifunguka kuhusu jinsi Victor alikuwa akimchunga sana wakati wakiwa pamoja.

"Vitu zenye ulikuwa ukinifanyia, ata sikudhani ungenipigia simu. Wewe umeniwekea mambo yenye ata sifanyi. Unaweza oa mwanamke asiongee na watu, ata asinunue kitu. Mimi sitaki mwanaume wa kuniwekea masharti. Nataka mwanaume wa kuniweka free," Anita alisema.

Pia alifunguka kuhusu jinsi mumewe alikuwa akimpiga mara kwa mara.

"Ananiwekea kikwazo vingi. Ananichunga sana. Nikitoka kazi alikuwa anasema nimetoka kwa wanaume. Mpaka niliacha kazi nikae kwa ndoa. Nikiwa nyumbani anasema naongea na jirani. Kuna mama wa ploti huwa anamwabia ata nikienda kwa duka. Hivyo hivyo unakula makofi. Unakula makofi mpaka kichwa inachanganyikiwa ata unashindwa kufanya kazi. Mimi nimechoka kupigwa,!" alisema.

"Kama ni unga, huwa ananunua mfuko moja. Huwa tunakula mara nne. Ukimwambia unga imeisha, anakuuliza imeisha aje? Anakwambia unakula sana. Ukimuitisha pesa anasema si uitishe hao wanaume. Na mimi sina wanaume. Mimi nimechoka na huyo mwanaume. Nilikuwa nampenda lakini apana. Mtu unampenda lakini anakupeleka kaburini," aliongeza.

Victor alijitetea akisema amejuta na hatawahi kurudia makosa yake.

Anita hata hivyo alisikika kushikilia msimamo wake kwamba hawezi kurudiana naye.

"Mimi vile nilitoka kwa nyumba sitawahi kurudi. Huyo mwanamke huwa anakwambia mambo ungekuwa umemleta kwa nyumba saai," alimwambia Victor.

"Mimi siwezi kurudiana naye. Nikimwambia anipeleke kwao, ananiambia nijipange nimpeleke kwetu. Kati yangu na yeye, nani ameoa mwingine," aliongeza.

Victor alisema, "Mimi nilimtoa kwa mwanaume. Nimekuwa nikifanya kazi, kila Jumamosi nimekuwa nikimpatia elfu moja anatumia mtoto wake. Huyo mwanaume amekuwa akimpigia simu hata tukiwa na yeye kwa nyumba. Nikijaribu kumwambia anakuwa juu. Haambiliki."

Huku akijibu, Anita alisema, "Huyo mwanaume nilikuwa na yeye kabla ya wewe. Na nikaachana na yeye kabla tupatane. Wachana na maisha yangu. Huwa unashinda ukinitishia eti utaninyonga. Kama huwa unanyonga watu mimi hutaninyonga."

Pia alitupilia madai ya kuwa na mimba akisema, "Kuna siku nilikwambia niko na mimba? Mimi niwe na mimba na sijui. Kuna siku umenipeleka kliniki. Sina mimba. Kama niko nayo sijui."

Katika maneno yake ya mwisho, Victor alimwambia Anita, "Mimi Anita nampenda na naomba arudi."

Anita alisema, "Nimemuacha abaki salama na huyo mwanamke wake wabaki salama."

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved