logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: Mwanadada aridhika baada ya mumewe kukubali kumsamehe licha ya kukiri ku'cheat

"Kuna vile nilimcheat kidogo. Nakubali makosa yangu nilimcheat ya ukweli," Emily alisema.

image
na Samuel Mainajournalist

Patanisho17 February 2025 - 09:00

Muhtasari


  • Emily alisema ndoa yake ya miaka mitano imekuwa na misukasuko tangu alipokanyaga nje ya ndoa, na mumewe akagundua.
  • Emily alisema angependa kumuomba msamaha mumewe, na kujua uamuzi wake ili ajue mustakabali wa ndoa yake.

Patanisho

Bi Emily Awuor mwenye umri wa miaka 24 kutoka Homa Bay alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mume wake John Juma (29) ambaye hajakuwa na mawasiliano mema naye.

Emily alisema ndoa yake ya miaka mitano imekuwa na misukasuko tangu alipokanyaga nje ya ndoa, na mumewe akagundua.

Alisema ingawa mumewe alisema amemsamehe, bado anahisi kama kwamba mambo yamebadilika.

“Mzee aliniruhusu kuenda kazi. Yeye akaenda kazi. Kuna vile alianza kushuku vitu kidogo kidogo. Alianza kushuku kuna mwanaume ananinyemelea kazini. Kutoka hapo haongei vizuri. Vile nilienda kazi, sijui alianza kushuku nini,” Emily alisimulia.

Aliongeza, “Kwa upande wangu naona nilimkosea. Kuna vile nilimcheat kidogo. Nakubali makosa yangu nilimcheat ya ukweli. Nilikubali makosa yangu, nikamuomba msamaha, na nikamuambia hiyo maneno nimeacha. Jamaa alikuwa kazi kwingine tulikuwa tunaongea na yeye. Vile nilienda kazi, mzee aligundua bado tunazungumza.”

Emily alisema angependa kumuomba msamaha mumewe, na kujua uamuzi wake ili ajue mustakabali wa ndoa yake.

“Bado tuko pamoja, alisema amenisamehe lakini vile anafanya, wakati  mwingine nikimpigia simu hashiki. Nilikubali makosa yangu mpaka nilimueleza kile kilifanya nifanye hivyo. Tuliongea lakini hatujakuwa tukizungumza vizuri. Ningependa kumuomba msamaha nijue uamuzi wake,” alisema.

Bw John alipopigwa simu, Emily alichukua fursa kuomba msamaha na kumuuliza mumewe kuhusu uamuzi wake.

“Nimejaribu kukuomba msamaha ni kama hujanisamehe bado. Ningependa kujua kama umenisamehe ya kweli ama kuna kitu bado inakuuma kwa roho,” Emily alimwambia mumewe.

John alimjibu,”Mimi nilikusamehe kitambo, sina kitu nimeweka kwa roho.. Mimi nataka tu ukuje nyumbani, sina maneno mingi.”

Katika maneno yake ya mwisho, Emily alimwambia, “Nimeshukuru kwa kunisamehea, sitawahi kurudia makossa tena. Nakupenda ndo maana nilikuleta Patanisho unisamehe Wakenya wote wakiskia.”

Je, una maoni ama ushauri gani kuhusu Patanisho ya leo?


Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved