
Amina Salmashir
22yrs kutoka Dandora hapa jijini Nairobi. Naomba mnipatanishe na Bwana yangu
Bilali Hashim 26yrs. Tumekuwa kwa ndoa kwa miaka miwili na tuko na Mtoto moja.
Nilikosana na Mume wangu miezi tano imeisha kwa sababu alisikiza maneno ya watu
sana mpaka tukawachana..
Katika kitengo cha Patanisho, Amina Salmashir (22) kutoka Dandora alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mume wake Bilali Hashim (26) ambaye alikosana naye mwaka jana.
Amina alisema ndoa yake ya miaka miwili ilisambaratika miezi mitano iliyopita kufuatia fitina za majirani kwa ploti.
Alisema mzozo wa kamba ya kuanikia nguo ulipelekea jirani kumshtumu kwa kum’cheat mumewe, jambo lililofanya Bilali amteme.
“Mume wangu alikuja, yeye mwenyewe akaanza kusema niko na wanaume wengine. Tulikuwa tumegombana na watu wengine mahali naishi, wakaanza kumwambia naleta wanaume wengine,” Amina alisema.
Aliongeza, “Tulikuwa tumekosania kamba ya kuanika nguo na jirano, nilikuwa nimeanika nguo za mtoto alafu jirani akaja kuniamuru nizitoe kwa Kamba. Bwanangu alikuwa kwa nyumba, huyo mama akaanza kusema niko na wanaume wengi. Mimi sikuwa kumcheat, ni ile tu maneno ya watu. Mtu aliwahi kuja ni kaka yangu mdogo, na ata yeye anamjua.”
Bw Bilali alipopigiwa simu, Amina alichukua fursa kuomba msamaha na kumshawishi arudi nyumbani.
“Mimi naomba msamaha. Wewe ulichukulia tetesi za jirani kuwa serious. Mtoto anakuhitaji. Mimi mwenyewe sina kazi niko tu kwa nyumba.Kila binadamu hukosea. Naomba turudiane tu kama zamani. Wewe ndiye baba mtoto wangu, hakuna mwanaume mwingine anaweza kuja kwa nyumba ila wewe,” Amina alimwambia mumewe.
Bilali alieleza kwamba anapanga kurudi na akasema ataweza kuzungumza na mkewe wakati huo.
Hata hivyo, alikiri kwamba ni kweli alikuwa ameondoka ili kuzuia kuchukua hatua mbaya baada ya kupata meseji za kutiliwa shaka kwenye simu ya mkewe.
“Nilikwambia nikitoka mahali niko nitakuja tuongee. Nikija Nairobi nitakuja tuongee. Nitarejea Nairobi wiki ijayo,” Bilali alimwambia mkewe.
“Nilimuacha kwa nyumba na kila kitu. Na rent bado nalipa. Kuna watu waliniambia anacheat lakini sijaichukulia hivyo. Niliona badala nikae hapo nimpige nikaondoka tu. Nilipata meseji hapo kwa simu yake. Kuna watu alikuwa anachat nao hapo kwa WhatsApp,” aliongeza.
Amina alisema, “Watu nilikuwa nachat na wao, lakini naomba msamaha, haitawahi kujirudia tena. Mimi nakupenda sana. Nilikuwa na stress. Wewe jua tu nakupenda, na wewe ndiye utabaki kuwa baba wa mtoto wangu.”
Kwa upande wake, Bilali alisema, “Niko pale kwa ajili ya kuangalia mtoto, na sitaki apitie shida. Ndio nimemsamehea, lakini kutoka kwa roho yangu itachukua muda kidogo.”
Je, una maoni ama ushauri gani kuhusu Patanisho ya leo?