logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jamaa ajawa wasiwasi baada ya shemejiye kutishia kumfukuza dadake kutokana na kosa lake

Reuben alisema shemejiye amekuwa akitishia dadake kwamba atamfukuza tangu alipoacha kazi hiyo.

image
na Samuel Maina

Patanisho26 February 2025 - 09:01

Muhtasari


  • Reuben alisema uhusiano wake na Shadrack uliharibika mwaka wa 2023 wakati aliacha kazi ambayo shemejiye huyo alikuwa amempea.
  • “Shida yangu ni kuwa dadangu anasema anamvuruga, anamwambia ataenda kama kakake aliacha vitu zake," Reuben alisema.

Watangazaji wa Radio Jmabo

Reuben Wanyonyi mwenye umri wa miaka 27 kutoka Bungoma  alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na shemeji yake Shadrack Simiyu (25) ambaye alikosana naye takriban miaka miwili iliyopita.

Reuben alisema uhusiano wake na Shadrack uliharibika mwaka wa 2023 wakati aliacha kazi ambayo shemejiye huyo alikuwa amempea.

Alieleza kwamba jambo hilo limeleta misukasuko kwenye ndoa ya dadake.

“Ilikuwa 2023, shemeji yangu alikuwa anafuga kuku. Aliniajiri akasema nifanye kazi. Nikafanya kwa miezi tatu, hakunipea pesa. Nikaamua kuachana na kazi. Shemeji akaona vibaya akaanza kuniuliza mbona naacha kazi. Shemeji alisema mradi tu nipate chakula pesa nyingine atanipea. Naona ni kama alitaka mradi nikule, nilale na nimfanyie kazi. Mimi niliona ni ngumu,” Reuben alisimulia.

Reuben alisema shemejiye amekuwa akitishia dadake kwamba atamfukuza tangu alipoacha kazi hiyo.

“Wakati nilienda akaona ni kama dadangu alifanya niache kazi. Kuanzia hapo hatuongei, dadangu ananipigia simu ananiambia shemeji anampeleka vibaya anasema atamfukuza kwa sababu niliacha mali yake na ni mimi tu alikuwa naye naweza kumfanyia kazi,” alisema.

“Nilitaka kumwambia niliacha kazi kwa sababu niko na mahitaji mengi. Niko na mtoto mdogo. Nataka ajue nilienda kwa sababu kazi haikuwa inanipea pesa ya kutosha na nisifanye aachane na dadangu, nisije nikawa wa kuwatenganisha,” aliongeza.

Shadrack alipopigiwa simu aliweka wazi kwamba Reuben alimkosea sana.

“Hiyo maneno niliachana nayo hivyo. Alinikosea sana nikaachana na hiyo maneno kabisa,” alisema kabla ya kukata simu.

Reuben alisema, “Shida yangu ni kuwa dadangu anasema anamvuruga, anamwambia ataenda kama kakake aliacha vitu zake akaenda. Dadangu akifanya kitu anaweka hapo jina langu. Dadangu amejaribu kuripoti kwa wazazi lakini shemeji anapatia baba kakitu mzee ananyamaza tu.”

Alipopewa nafasi ya kumwambia shemejiye ujumbe wa mwisho, Shadrack alimwambia, “Shadrack, kazi sikuacha kwa ubaya kwa sababu ile pesa ulisema utanipea sikuacha kwa ubaya. Isiwe ni mimi nitafanya mkosane. Kama nilikukoea naomba unisamehe na muendelee na maisha yenu vizuri.”

Je, una maoni ama ushauri gani kuhusu Patanisho ya leo?

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved