
Jamaa aliyejitambulisha kama Tony Omondi (25) kutoka Siaya alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mpenzi wake Faith Naunga (26) ambaye alikosana naye hivi majuzi.
Tony alisema uhusiano wake wa miaka miwili ulianza kuyumba baada ya mpenziwe kurudi kwao jijini Mombasa.
“Tumekuwa kwa mahusiano miaka miwili. Tulikuwa tukichumbiana tukipanga kuoana. Mambo imekuja ikabadilika. Alirudi Mombasa hivi majuzi. Nimekuwa nampigia simu hapokei. Amekuwa akijua tunapanga kuoana,” Tony alisema.
Aliongeza, “Naomba aniambie msimamo wake ili nijue hatua ya kuchukua.”
Faith alipigiwa simu lakini akakata pindi baada ya kufahamishwa anatafutwa na Tony.
Tony alisema kwamba hatua ya mpenziwe huyo ni thibitisho tosha kwamba hamtaki.
“Nimekubali matokeo juu siwezi lazimisha. Kuanzia mwanzo tulikuwa tunapendana. Nilikuwa namtumia tiketi ya kutoka Mombasa kuja Mombasa, na akakuja. Ni msichana wa Kipwani. Nilikuwa tu hali ya kikazi huko Mombasa tulipojuana lakini kazi ikaja kuisha. Huwa nang’ang’ana kimwanaume ilimradi tu apate chenye anataka,” Tony alisema.
Alifichua kwamba mwanadada huyo tayari amemblock kwenye laini zake zote.
“Nimeridhika. Hiyo ni dhibitisho tosha kwamba hataki mambo na mimi. Namba zangu zote ameziblock. Juzi nilimpigia na namba hajui, kuskia sauti yangu akakata. Hakuna kitu nilimfanyia. Nilikuwa tayari kumuomba msamaha. Kama imekataa, ibaki hivyo,” alisema.
Je, una ushauri ama maoni gani kuhus Patanisho ya leo?