
Kijana aliyejitambulisha kama Benson Agumba Opiyo (25) kutoka Kakamega alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Irene Weke (23) ambaye alikosana naye mwezi uliopita...
Benson alifichua maelezo ya kutisha kwamba mkewe alienda nyumbani kwao na kukataa kurudi baada yay eye kujaribu kujitoa uhai kwa kunywa sumu.
“Tulipatana mwaka jana mwezi wa tano, tukaamua tuishi pampja. Tulikuwa tunaishi tu vizuri. Alikuwa aende nyumbani mwezi wa kumi na moja mwaka jana, nikamtafutia nauli aende lakini hakuenda. Mwaka huu mwezi wa pili ndiyo aliamua anataka kuenda, nikamruhusu aende. Kuenda ndo akakataa kurudi. Lakini sasa ako Nairobi na amekataa kurudi,” Benson alisema.
Kijana huyo alidai kwamba alijaribu kujitoa uhai baada ya mkewe kumwambia kwamba hamtaki.
“Nilijaribu kujiua mbele yake. Nilikunywa sumu. Hadi mwenyewe aliniambia ameniogopa. Nilipelekwa hospitali ndio maana sikukufa. Nilikuwa nampenda, tulikuwa tunaishi pamoja, alafu ananiambia hanitaki,” alisema.
Aliongea, “Sasa najuta sana na sitawahi kurudia kitu kama hiyo. Huwa tunaongea lakini hapo kwa kurudi ndo hataki. Aliniambia alinishtuka kama naweza fanya kitu kama hiyo. Nataka nimuombe msamaha nione kama atarudi. Akikataa nitakubali, sitafikiria mambo kama hiyo nilijaribu.”
Irene alipopigiwa simu alisisitiza kwamba anahitaji muda wa takriban wiki mbili ili kumaliza kazi kabla ya kurudi katika ndoa yake.
Benson alimwambia, ”Huo muda anaweza punguza? Nikimpea ile pesa anahitaji ya mtoto atarudi?... Nataka unihakikishie mbele ya Wakenya kama unanipenda kweli. Mimi nakupenda. Na ile kitu nilifanya sitawahi kurudia.”
Irene aliibua wasiwasi kuhusu mahitaji ya kifedha kuona kwamba mpenziwe hana kazi.
Pia alikiri jinsi tukio la mumewe kujaribu kujitoa uhai lilimfanya aingiwe na hofu.
“Inafikanga muda hana kazi. Sasa mimi ndiye nahusstle. Kitu ilinishtua, alikuja akakunywa dawa. Kumuuliza akasema ananipenda ndiyo maana anakunywa dawa. Juu nilikuwa nimemwambia naenda nyumbani. Sasa hiyo kitu ikaniogopesha sana. Nilimbeba nikampeleka hospitali. Pesa nilikuwa naenda nayo nyumbani ndiyo nilitumia kumpeleka hospitali,” alisema.
Benson alisema ,’Aliniambia hanitaki, hiyo ndiyo ilifanya nikunywe dawa.. Acha nijikakamue nikuwe na kazi alafu urudi tuendelee na maisha.”
Katika maneno yake ya mwisho kwa mpenziwe, Irene alimwambia, ‘Nakupenda. Kama sikupendi singekuwa nakuongelesha. Naomba ubadilike tabia na ukuwe kama mwanaume, tutaishi vizuri.”
Je, una ushauri ama maoni gani kuhusu Patanisho ya leo?