Danstan Wanjala (24) kutoka Kitengela alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Jackline Kasinda (23) ambaye alikosana naye hivi majuzi.
Wanjala alisema ndoa yake ya miaka miwili iliharibika baada ya yeye kutumia pesa kwa njia ambayo haikumfurahisha mkewe.
Alisema tangu wakati huo hawajakuwa wakizungumza vizuri kwa nyumba na amekuwa akipika chakula na mkewe hali.
“Juzi nilipata pesa kidogo nikaona nilipe simu yangu juu ni ya M-kopa. Yeye alikuwa amepanga kufanyia pesa kitu ingine. Vile alikuja jioni akajua vile nimetumia pesa. Akaniuliza kwa nini nililipa simu na alikuwa amepangia hiyo pesa. Mimi sikujua kuna matumizi mengi alikuwa anataka kufanyia pesa,” Wanjala alisema.
Aliongeza, “Hivyo ndo alinyamaza.Sasa tukiwa kwa nyumba hatuzungumzi. Hapo awali akienda kazi alikuwa ananiambia goodbye bebi, sasa haniambii. Mimi ndiye huwa napika kila siku juu huwa anatoka kazi kuchelewa. Tangu tukasirikiane, sio rahisi akule lakini akipata anakula. Jana nilipika ugali na omena, nikangoja aje tule. Alipofika akasema ameshiba.”
Jackline alipopigiwa simu, alisisitiza kwamba alikasirika kuhusu maamuzi ya kifedha ya mumewe.
“Tulikuwa tumechukua pesa kujenga nyumba jioni. Badala hiyo pesa apate tulipe nusu, yeye alilipa simu,” Jackline alilalamika.
Wanjala alijitetea kwa kusema alihofia simu yake kuzimwa.
Jackline alimwambia, “Hapo ulifanya makossa ungekuja uniambie umepata pesa fulani tupange vile tutatumia. Hiyo pesa ungepeana kwa loan.”
Wanjala alilalamika kuhusu jinsi amekuwa akijaribu kumfurahisha mkewe na haskii.
“Nimepika ugali na kuku ili ufurahie, lakini hukufurahia. Jana nikapika ugali na omena ndo ukuje ukule, na hukula.. Jioni nikienda kwa nyumba tutaongea tujue vile tutalipa hiyo pesa. Nisamehe kama nimekosea. Fanya moyo wako uwe mwepesi ndiyo unisamehe. Sitarudia,” alisema.
Jackline alikubali kumsamehe na kumhakikishia kuhusu upendo wake kwake.
“Mimi sina ubaya na wewe. Nampenda, tutarudi kukaa vile tulikuwa tunakaa hapo nyuma lakini asirudie hiyo makosa,” alisema.
Je, una ushauri ama
maoni gani kuhusu Patanisho ya leo?