

Kipsang Cheruiyot (28) kutoka Kericho alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Margaret Muriuki (26) ambaye alikosana naye mwezi uliopita.
Kipsang alisema ndoa yake ya mwaka mmoja ilisambaratika wakati mkewe alitoroka na kurudi kwao Nyeri baada ya kuchoshwa na tabia yake ya ulevi.
Alisema kwamba mama huyo wa mtoto wake alikuwa amechoshwa na mtindo wake wa kushuka nywele.
"Mke wangu, nilikuwa nakunywa sana na hakuwa anataka. Alikuwa ananiambia niachane na pombe na siachi. Nilikuwa nakunywa naingia kwa nyumba kuchelewa, akachoka akaenda kwao," Kipsang alisema.
"Sasa nimepunguza ulevi kiasi. Huwa naongea na yeye ananiambia niendelee na pombe yangu. Pia alikuwa ananiambia niachane na mambo ya kushuka nywele. Nilikuwa nimeweka dreadi anauliza tunashuka nywele sote wawili kivipi? Hakuwa anataka hiyo mambo ya kushuka nywele. Nimemuoa lakini sijawahi kuenda kwao. Sina cheti cha ndoa," aliongeza.
Margaret alipopigiwa simu, Kipsang alitumia fursa hiyo kuomba msamaha na kumsihi warudiane.
Mwanadada huyo ambaye alisema yuko kazini alisema kwamba angempigia simu mpenizwe baadaye. Hata hivyo, alisema kuna uwezekano wa wao kurudiana.
Kipsang alisema kwamba yuko tayari kuacha pombe na hata kuweka nywele fupi..
"Nitaachana na pombe ata nitaenda kanisa. Ata mambo ya nywele niliachana nayo. Alisema naharibu pesa. Sasa nimenyoa kipara," alisema Kipsang.
Je. una maoni ama ushauri gani kuhusu Patanisho ya leo?