
Katika kipindi cha Patanisho kwenye stesheni ya Radio Jambo, jamaa kwa jina Steven kutoka Kitale aliomba kupatanishwa na mkewe ambaye walikosana baada ya kukaa kwenye ndoa ya miaka 3.
Steven alieleza kwamba anahisi kabisa yeye ndiye alimkosea mkewe kwa hulka yake ya kukurupukia simu yake kila mara ilipokuwa inapigwa.
Alisema kwamba kila mara simu ya mkewe ilipokuwa inapigwa,
alikuwa anataka kujua ni nani huyo aliyekuwa anampigia, jambo ambalo
lilionekana kumkasirisha mkewe.
“Tulikuwa tunaishi kwa
ndoa miaka 20, tulianza kuchumbiana 2021 tukakuwa tukivurugana tu mambo ya
simu. Mtu akimpigia nilikuwa nataka kujua ni nani anampigia na kwa kweli mimi
ndiye nilikuwa mwenye makosa. Hilo ni kama lilimkasirisha. Alitoka yuko mahali
anafanya kazi na huwa tunaongea lakini nahisi nilimkosea nataka ajue kwamba
bado nampenda,” Steve alisema.
Betty Wanyonyi kwa upande wake alithibitisha kwamba ni kweli
tabia ya mumewe kurukia simu yake ndiyo iliyomfanya kuchukua uhusiano wao na
kutaka kuivunja.
“Mimi ni yule ninauza kwa
duka, mteja akipiga simu kuulizia kuhusu bidhaa huyo mume wangu anaanza kuhisi
kwamba ninamsaliti katika mapenzi. Kila wakati mwenye anapigac simu anataka
kuona ni nani na hicho ndicho kilinifanya nikakasirika.
“Hata kama kuna wale
wateja ambao wanajaribu kunitongoza nilikuwa nawaambia kwamba nimeolewa,” Betty alijieleza.
“Nataka tu kukuomba msamaha na hata hayo mambo
ya simu sitawahi shika simu yako hata siku moja,” Steven alinyenyekea akisisitiza
kuikwepa kabisa simu ya mpenziwe.
Baada ya tathmini ya muda, Betty alitamka kwamba amemsamehe
huku Steven akieleza furaha yake baada ya kusamehewa na mpenzi wake.